Ijumaa, 28 Juni 2024

Mambo mapya saba, Sabasaba 2024

 Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com

Ni msimu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Sabasaba, safari hii yakiwa ni ya 48 tangu kuanzishwa kwake, yakiendeshwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara  Tanzania (Tan Trade), ambapo kwa mwaka huu ykuna mambo saba tofauti, mapya yanayobeba maonyesho hayo ikiwamo matumizi ya robot (akili bandia (IA).

Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis

Katika mahojiano, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Latifa Khamis ameeleza kuwa maonyesho ya mwaka huu ni tofauti na miaka mingine, kutokana na ukweli kwamba yanabebwa na mambo saba tofauti.

“Maonyesho ya mwaka huu yana sura ya kipekee, tuna bidhaa za kitanzania halisia, tuna nchi za kigeni zaidi ya 25 zinashiriki, tuna mabanda manne ya kimataifa, tuna nchi zaii ya sita zitahimisha siku za mataifa yao kwa mwaka 2024 kipindi cha maonyesho, tiketi za Sabasaba mwaka huu zipo kwa mtandao;

Pia tutawadhamini wafanyabiashara wa Kariakoo ili waweze kuuza bidhaa za jumla kutoka kwa washiriki wa maonyesho kutoka nje ya nchi, lakini zaidi tutakuwa na roboti atakayetumika kukaribisha mgeni rasmi. Hii itaonyesha namna teknolojia ilivyokua na inavyoweza kutumika kuleta maendeleo,” amesema Latifa.

Kuhusu kuwadhamini wafanyabishara wa Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo wa TanTrade amesema kuwa, watafanya hivyo kwa lengo la kundi hilo kuachiwa bidhaa na washiriki wa nje, ambao mara nyingi huondoka na bidhaa zao wakishamaliza maonyesho.

Kwa mujibu wa Latifa nchi zitakazoathimisha siku za mataifa yao kwenye maonyesho ya Sabasaba ni pamoja na China, Uturuki, Singapore, Pakistan, Ghana, Uturuki na Korea.

Amesema kwamba maonyesho hayo yanachangia pato la taifa kwa kuwa washiriki wa nje wanalipia ushiriki wao, lakini pia yanakuza diplomasia kati ya Tanzania nan chi washiriki.

Latifa ameeleza kuwa kwa mwaka huu 2024, nchi za China na Misri zinaongoza kwa kuleta washiriki wengi, China ikiwa na washiriki zaii ya 300 na Misri ikiwa na washiriki 35,

Kuhusu ushiriki wa Tanzania mkurugenzi huyo amesema, katika maonyesho hayo yaliyoanza leo yakitarajiwa kukamilika Julai 13, wizara na taasisi 2,979 zinashiriki huku kampuni zikiwa 223.

Latifa amesema katiuka maonyesho hayo Zanzibar ina washiriki zaidi ya 15, akieleza kuwa lengo la maonyesho hayo ni kuongeza ustawi wa jamii akibainisha wanafunzi na mama lishe nio walioongoza kwa kupata ajira.  

Amesema kupitia maonyesho hayo TanTrade inaendesha mpango maalum wa Urithi Wetu inayojumuisha watoto hasa wa vijijini ambao hupewa nafasi ya kutembelea maonyesho hayo kwa siku tatu nan je ya maonyesho hayo kujifunza masuala ,mbalimbali kwa lengo la kuwarithisha mema ya taifa.

“Kwa mwaka huu tuna Watoto kutoka Monduli mkoani Arusha, Kondoa Mkoa wa Dodoma, Kilosa mkoani Mrorogoro, pia kutoka Unguja na Pemba,” amesema Mkurugenzi huyo wa TanTrade.

 

Ijumaa, 21 Juni 2024

Nape: Wadau naomba tuaminiane

Selemani Msuya, daimatznews@gmail.com

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amewaomba wadau wa sekta ya habari kuwa na imani naye kuhusu vifungu 12 vinavyolalamikiwa katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Mnauye

Kauli hiyo ya Waziri Nape imetokana na maazimio sita yaliyosomwa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Thobias Makoba, ambapo moja ya azimio lilikuwa ni vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari ambavyo vinalalamikiwa na wadau wa sekta hiyo.

Nape ametoa kauli hiyo wakati akifunga Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari lilifoanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kwa siku mbili na kushirikisha wadau zaidi 1,200 kutoka sekta umma na binafsi kwenye tasnia ya habari.

"Nitatoa mfano, hoja ya umiliki wa vyombo vya habari, ipo kwenye Sera ya Vyombo vya Habari ya mwaka 2003, mimi sikuwepo, nilikuwa ndio naanza kazi CCM. Jamani naomba tuaminiane, mimi ni mdau wa sekta hii kwa sababu nimeisomea. Sitengenezi kwa ajili yangu au ajili yenu, ni kwa ajili yetu, kwa sababu sijui watoto wangu watafanya kazi gani. Tuaminiane. Tutafika salama;

“Hili suala la vifungu 12 vya Sheria ya Huduma ya Habari mnavyovitaja kila mara, nadhani nimefafanua sana kwamba hoja hizi tutazifanyia kazi, baada ya sera mpya kutungwa na vingine vitaingia kwenye kanuni, najisikia vibaya kwa sababu tumefanya vikao na kukubaliana,” amesema.

Awali, katika maelezo yake, Makoba alitaja maazimio mengine kuwa ni wizara na taasisi za Serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari ifikapo Desemba 24 mwaka huu 2024 na wamiliki waweze kulipa mishahara.

Jingine ni Serikali kuangalia uwezekano wawekezaji wakigeni kuwa na asilimia 75 ya umiliki vyombo vya habari, vyombo vya habari kuandika habari za kijamii, vyombo vya habari vitoe fursa sawa kwa vyama vyote na vyombo vya habari vya mtandao viongoze ubunifu na kuandaa maudhui yenye tija na kujijengea uaminifu kwa walaji.

Hata hivyo, Waziri Nape amesema kwamba amekuwa akisikitishwa na mwendelezo wa kulalamikia vifungu 12 vya sheria hiyo, huku akiwa ameelezea kwa nini havikufanyiwa mabadiliko wakati wa mabadiliko yaliyohusisha vifungu tisa pekee vya sheria hiyo.

Amesema kuna vifungu vinavyohitaji mabadiliko ya sera ndipo viweze kubadilika na vingine vitaingizwa kwenye kanuni, hivyo amewataka wadau kuacha kulalamika wakihisi Serikali haitaki.

Nape amesema katika mchakato huo wa kubadilisha sheria aliwashirikisha baadhi ya waandishi na kuwaonesha hali halisi, hivyo anaumia pale ambapo anatiliwa mashaka katika hilo.

Ameeleza kwamba aliwasilisha sheria bungeni na mjadala ukawa mkali kwa wabunge kutaka mabadiliko na alikubali  mabadiliko ambayo wabunge walitaka, jambo  ambalo halijafanywa na waziri yoyote.

“Sikilizeni mimi naipenda sekta hii, kiasi kwamba 2017 nilikuwa tayari kupoteza uwaziri, kulinda uhuru wa vyombo vya habari wa nchi hii, msisahau rekodi hizi.

:Sekta ya habari ipo ndani ya moyo wangu, siku ile wakina Deudatus Balile, Jesse Kwayu na wengine wanaenda kusoma ripoti nilijua nafukuzwa, waliniambia nitafukuzwa nikawaambia nilipofikia siwezi kurudi nyuma, uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kuliko kazi yangu," amesema Nape Napa.

Ameongeza: "Siwezi kuingi kwenye rekodi ya kuhujumu vyombo vya habari kwa sababu utanifuata maisha yangu yote, kwa sababu ya cheo tu. Si nilitoka, leo nimerudi nasonga mbele na heshima yangu ipo. Wanahabari msisahu, sekta ya habari ipo mikono salama. Na wao wanajua, wasioitakia mema sekta hii wanajua, ilimradi Nape yupo atasimamia na wanahabari wake.” 

Nape amewahakikishia wadau wa sekta ya habari kuwa serikali chini ya uongozi Rais Samia Suluhu Hassana ina dhamira ya kweli ya kujenga ushirikiano, ili kuhakikisha kila upande unanufaika.

Jumatatu, 17 Juni 2024

Msikiti 'mikononi' mwa RITA Arusha

Mwandishi Wetu, Arusha

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini nchini (RITA), umeunda kamati ya muda itakayochukua majukumu  ya Bodi ya Udhamini iliyomaliza muda wake ya Taasisi ya Arusha Muslim.
Sanjari na hatua hiyo, RITA imeunda Kamati ya Maalumu ya Uchunguzi itakayofuatilia malalamiko ya wanachama, kuwatuhumu viongozi wa msikiti huo kuhujumu mali za  taasisi hiyo.

Akizitambulisha kamati hizo katika kikao kilichojumuisha uongozi wa RITA, viongozi wa Serikali ya Wilaya ya  Arusha, viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA ), viongozi wa Arusha Muslim pamoja na wanachama wa msikiti huo, Kabidhi Wasii  Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi ameziagiza kamati hizo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu.

 “Nimeiagiza Bodi iliyomaliza muda wake kuwasilisha RITA taarifa ya mapato na matumizi,” amesema Kanyusi na kuiagiza kamati ya mpito kuhakikisha inafanya marekebisho ya katiba na uchaguzi unafanyika ndani ya siku 60, ili kupata viongozi watakaosimamia taasisi kwa mujibu wa katiba.

Kanyusi pia ameaitaka Kamati Maalumu ya Uchunguzi kukamilisha kazi iliyopewa ndani ya siku 14 na kuwasilisha taarifa ya uchunguzi RITA.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha, Khamana Simba  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo kwenye kikao hicho, amewataka wanachama wa Arusha Musilim kuwa watulivu na kwamba Serikali ipo pamoja nao kuhakikisha mgogoro huo wa muda mrefu unapata ufumbuzi wa kudumu kwa amani, utulivu na haki.

“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan inafuatilia kila kitu na ninawahakikishia kwamba, ufumumbuzi wa tatizo lenu utapatikana,” amesema katibu tawala huyo na kuwataka waendelee kuwa wamoja na watulivu.

Baadhi ya wanachama  ARUSHA Muslim,  Mustapha Mohamedi na Kassim Collins waliipongeza Serikali  kwa kufuatilia mgogoro huo huku wakiomba hatua zichukuliwe kwa watakaobainika kuwa wamefanya ubadhirifu.

Naye, Naibu Kabidhi Wasii Mkuu, Irene Kesulie aliwatoa hofu wanachama wanaoidai taasisi hiyo  kwamba wafuate taratibu ikiwemo kuandika barua na kuziwasilisha RITA ili taratimu za kisheria ziweze kufuatwa na wapate haki yao.

“RITA kama ipo hapa kusimamia haki za wanachama kwa wa sheria na katiba. Tunawasihi endeleeni kuwa watulivu na wavumilivu,” amesema Irene.

Alhamisi, 13 Juni 2024

INEC: Wanasiasa someni Sheria ya Uchaguzi msipotoshe wananchi

Na Selemani Msuya 

WAKATI vyama vya siasa vikiitaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa, tume hiyo imevishauri vyama hivyo vikasome Kifungu cha 10 (1) (C) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ili viache kupotosha wananchi.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa INEC, Ramadhan Kailima wakati akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya kwanza kwa waandishi wa habari 250 leo Juni 13, jijini Dar es Salaam.

Kailima amesema kumekuwa na muendelezo wa viongozi wa vyama vya siasa kuitaka INEC isimamie uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa hoja kwamba Sheria ya Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi inataka hivyo, jambo ambalo sio kweli.

"Waandishi wa habari nyie ni watu muhimu sana kwenye mchakato wote wa uchaguzi, sisi INEC, wanasiasa na wananchi wanawategemea mtoe bahari zenye usahihi, naomba hili la wanasiasa kutaka sisi tusimamie uchaguzi mliandike kwa usahihi kwani kwa sheria iliyopo sasa hatuna mamlaka hiyo hadi Sheria itungwe na Bunge.

Kifungu namba 10(1)(c) kinasema kwa kuzingatia matakwa  ya Ibada za 74(6), 75 na 78 ya Katiba, Tume itakuwa na majukumu la kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Serikali za Vijijini, Mitaa na Vitongoji Tanzania Bara kwa kuzingatia utaratibu utakaoainishwa katika sheria itakayotungwa na Bunge," amesema.

Mkurugenzi huyo amesema pamoja na kifungu hicho wanasiasa wameamua kupotosha, hivyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia taaluma yao kueleza ukweli ili jamii isipotoshwe.

Akizungumzia uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Kailima amesema zoezi hilo linaendeshwa kwa Kifungu 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba moja ya mwaka 2024, Kifungu cha 10(1)(a) cha Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba mbili ya mwaka 2024.

Pia amesema masharti ya vifungu rejewa yanaitaka INEC kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili kati ya uchaguzi mkuu uliomalizika na kabla ya uteuzi wa wagombea wa uchaguzi mwingine na masharti ya Ibara ya 74(6) ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Kailima amesema katika kutekeleza sheria na masharti hayo wanatarajia kuandikisha wapiga kura wapya milioni 5, 586,433 sawa na asilimia 18.7 ya wapiga kura milioni 29,754,699 waliopo kwenye daftari, baada ya uboreshaji uliofanyika 2019/20, huku wapiga kura milioni 4,369,531 wakitarajiwa kuboreshewa taarifa zao.

"Wapiga kura 594,494 2 wanatarajiwa kuondolewa kwenye daftari kwa kukosa sifa za kuendelea kuwepo kwenye daftari, hivyo baada ya uboreshaji INEC inatarajia kuwepo wapiga kura milioni 34, 746,638," amesema.

Mkurugenzi huyo amesema kutakuwa na vituo 40,126 vya kuandikisha wapiga kura, ambapo vituo 39,709 vitakuwa Tanzania Bara na 417 Zanzibar ikiwa ni ongezeko la vituo 2,312, ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika mwaka 2019/20.

Kailima amesema INEC imeweka mifumo ambayo inaruhusu Watanzania wenye sifa na wanaomiliki simu janja kuanzisha mchakato wa kujiandikisha au kuboresha taarifa zake kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Amesema mkakati wa INEC ni kuona wananchi wanaotumia simu ambazo sio janja yaani jina maarufu Viswaswadu nao kuanza kufanya mchakato wa kujiandikisha kabla ya kufika kwenye kituo cha kujiandikisha kumalizia zoenzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jocobs Mwambegele amewataka waandishi WA habari kutumia kalamu zao kutoa elimu ya mpiga kura, ili kila mwananchi aweze kushiriki uchaguzi.

"Tumewaita hapa kwa sababu ili haya ambayo tunafanya yaonekana kalamu zenu ndio zinaweza kuonesha kwamba INEC na wadau wake wanafanya kazi, hivyo tunaomba msikubali kupotosha jamii, simamieni taaluma zenu," amesema.

Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kutumia kituo cha kutoa huduma, pale ambapo watakuwa na changamoto za uandikishaji au uboreshaji wa taarifa zao.

Naye Mjumbe INEC, Jaji Asina Omari amesisitiza kuwa ufanisi wa tume hiyo utaonekana kupitia vyombo vya habari na kuwataka waandishi kushirikiana nao ili lengo la kuwa na uchaguzi wenye tija liweze kufanikiwa.

Dar mpaka Moro moto SGR abiria kuanza safari kesho

 

Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com

Dar mpaka Moro, hayawi, hayawi, sasa yamekuwa. Tanzania inaandika historia mpya katika nyanja ya usafiri na usafirishaji Saa12 kamili ya Juni 14, 2024, ambapo Treni ya Mwendokasi (SGR) inayotumia umeme, ikianza safari zake kwa kubeba abiria kibiashara.

Treni ya Umeme ya SGR

Treni hiyo itaanza safari zake, kabla ya muda uliopangwa wa Julai mwaka huu kufika, ambapo itaanza kwa safari za Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Nauli kwa abiria mmoja kwa kila safari ni Sh13,000 mtu mzima huku watoto wenye umri zaidi ya miaka minne wakitakiwa kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima.

Daima Tanzania blog, ilikuwepo kwenye kituo kikuu cha treni hiyo maeneo ya Steshen", ambapo ilishuhudia maandalizi ya mwisho yakiendelea, huku wananchi waliojaa bashasha, wakiingia na kuulizia upatikanaji wa tiketi.

Hata hivyo, walielezwa kuwa wanaweza kupata titeki hizo kupitia mtandao wa TRC au wawahi kufika kituoni hapo kabla ya muda wa safari.

Ratiba iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), inaonyesha kwamba treni ya kwanza ya Dar mpaka Moro, itaanza safari saa 12 kamili asubuni ambapo itasafiri kwa takriban dakika 109 kukamilisha safari yake.

Dakika hizo 109 ni sawa na saa 1 na dakika 49, ikimaanisha kwamba kwa mara ya kwanza abiria wa SGR, watafikishwa mjini Morogoro saa 1 na dakika 49.

Treni ya kwanza ya SGR kutoka Moro itaanza safari yake saa2:50 asubuhi na kuwasili Dar saa 4:39, huku treni ya pili kwenda Moro ikitoka Dar saa10 kamili jioni na itafika Moro saa 11:49.

Safari ya nne na ya mwisho kila siku katika ratiba ya safari hizo, itakuwa ikianzaia Moro kwenda dar, ambapo itaondoka saa 1:30 usiku na kuwasili Dar saa 3:19 usiku.

Kwa mujibu wa TRC, safari za treni hiyo zitafanyika kila siku, kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.

VAR kutumika Ligi Kuu msimu ujao

 Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amelifahamisha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa msimu ujao Ligi Kuu Tanzania, itaanza kutumia VAR.

Mashine ya VAR

VAR ni mfumo wa usaidizi kwa waamuzi wanapochezesha soka uwanjani kutumia 'video'.

Dk. Nchemba ametoa maelezo hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2024/2025 bungeni, mjini Dodoma leo, ambapo amesema lengo la kutumia mfumo huo ni kuhakikisha matokeo yanayopatikana yanakuwa ya haki.

"Msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania, tutaanza kutumia ''VAR'' ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki ,"amesema Dk.Mwigulu na kuongeza:

"Maana kuna timu zimezidi - msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa."

Waziri wa Fedha, amesema kuwa ili kuwepo na ''VAR'' za kutosha katika viwanja vyote, anapendekeza  Bunge litoe msamaha kwenye uingizaji wa mashine hizo na vifaa vyake.

"Ufafanuzi utakaotolewa hapo baadae, INAWEZEKANA," amesisitiza Dk. Mwigulu

 Kuhusu ubora wa eneo la kuchezea  kwenye viwanja mbalimbali, Dk. Mwigulu amesema tayari Serikali ilitunga sheria inayotoa msamaha kwenye uingizaji wa nyasi bandia na vifaa vyake. 

Bajeti; Malengo yake saba kiuchumi ni haya

 Exuperius Kachenje,daimatznews@gmail.com

Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, ametaja shabaha saba za uchumi kwa jumla katika bajeti yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
Begi la Bajeti ya Serikali mwaka 2024/2025

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2024/25, bungeni mjini Dodoma leo Juni 13, 2024, Dk. Mwigulu amesema shabaha hizo zimetokana na nyaraka na miongozo iliyozingayowa katika uandaaji bajeti hiyo. 

"Shabaha za uchumi jumla ni saba kama ifuatavyo; Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kufikia asilimia 5.4 mwaka 2024 kutoka ukuaji wa asilimia 5.1 mwaka 2023; Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimia kati ya 3.0 - 5.0 katika muda wa kati," amesema Dk Mwigulu.

Nyingine ni mapato ya ndani kufikia asilimia 15.8 ya Pato la Taifa mwaka 2024/25 ikilinganishwa na matarajio ya asilimia 15.4 mwaka 2023/24; Mapato ya kodi kufikia asilimia 12.9 ya Pato la Taifa mwaka 2024/25 kutoka matarajio ya asilimia 12.6 mwaka 2023/24 na kuwa na nakisi ya bajeti ikijumuisha misaada isiyozidi asilimia 3.0 ya Pato la Taifa.

Wabunge wakifuatilia hotuba ya bajeti ikisomwa bungeni mjini Dodoma, Juni 13,2024.

Kwa mujibu wa Waziri huyo wa Fedha, shabaha nyingine ni kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne. 

Bajeti hiyo inawasilishwa na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa Ibara ya 137 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na Kifungu cha 23 (3) cha Sheria ya Bajeti, Sura 439 na Kifungu cha 124 (4) cha Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Februari 2023.

Katika hotuba yake Dk. Mwigulu aliomba Bunge lipokee, lijadili na kukubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2024/25 yanayofikia Sh 


Kikokotoo sasa asilimia 40, Rais awapoza wastaafu

Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com

Serikali imesikia kilio cha wastaafu kuhusu kikotoo, ikitangaza kwamba malipo ya mkupuo sasa yatakuwa ni asilimia 40 kutoka 33 ya awali kuanzia mwaka ujao wa fedha.

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa bungeni mjini Dodoma leo Juni 13, 2024 na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba(pichani juu), alipokuwa akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

“Serikali imesikia kilio cha watumishi na kufanyia kazi suala la masilahi..., Rais Samia ameelekeza kuongezeka kwa malipo ya mkupuo....; 

"Wastaafu waliokuwa wakipokea asilimia 25 hadi 33 kwa malipo ya mkupuo, sasa watapandishwa hadi asilimia 35 na walioathirika na mabadiliko yaliyojitokeza watakuwa sehemu ya mabadiliko hayo," amesema Mwigulu na kuongeza:

“Serikali itaendelea kuliangalia kwa karibu suala la masilahi ya wastaafu kwa kuzingatia tathmini ya uhai na uendelevu wa mifuko yetu.” 

Hatua hiyo ya Serikali inagusa watumishi walioshushiwa malipo ya mkupuo kutoka asilimia 50 hadi 33 mwaka 2017 na kuzua manung'uniko kutoka kwa wafanyakazi, wakitaka mfumo wa zamani urejeshwe, ambapo kwa muda mrefu waliodai malipo hayo hayaendani na hali halisi ya maisha.

Hata hivyo, swali linalobaki kwa wastaafu ni namna watakavyopokea mabadiliko hayo ya kikokotoo, ambacho sasa malipo ya mkupuo yameongezeka kwa asilimia saba.Kabla ya kutangaza ongezeko hilo la malipo ya mkupuo kwa wastaafu, Waziri wa Fedha alieleza:

"Katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita, Serikali imelipa Sh. bilioni 160.04 kwa ajili ya kugharamia upandishwaji wa vyeo kwa watumishi wa umma  126,814 wa kada mbalimbali. Hata hivyo, kumekuwa na kilio kikubwa kutoka kwa wastaafu kuhusu kikokotoo; 

Kama asemavyo Naibu Waziri wa Fedha Mheshimiwa Chande kuwa mara zote mtoto akilia, mama hujua kwa sauti kuwa hapo mtoto analilia nini. Akilia anasema hapo ameshiba, akilia anasema hapo ana usingizi, akilia anasema hapo nguo zimembana au akilia anasema apelekwe hospitali; 

Serikali yetu sikivu inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan, imesikia kilio hicho na imekifanyia kazi kwa maslahi mapana ya wastaafu wetu na wanaotarajiwa kustaafu; ...Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza kuongezwa  malipo ya mkupuo kutoka asilimia 33 iliopo  sasa hadi asilimia 40."

Kwa mujibu wa Dk. Mwigulu hilo ndilo kundi kubwa la watumishi, wanaofanya kazi nzuri zaidi kwa taifa akiwataja walimu, kada ya afya, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na makundi mengine yalioko Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. 

"Rais ameelekeza kuongezewa zaidi kundi lililokuwa likipokea asilimia 25 hapo awali na kupandishwa kwenda asilimia 33, sasa itakuwa asilimia 35 kuanzia mwaka wa fedha huu. Watumishi walioathirika na mabadiliko haya watazingatiwa katika mabadiliko haya. 

Jumanne, 11 Juni 2024

Serikali yatoa msimamo Sekta ya Posta Afrika

Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha

Serikali ya Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Posta Afrika (PAPU), msimamo wake usioyumba kwamba, itaendelea kuunga mkono na kusaidia mikakati ya umoja huo kwa maendeleo ya Sekta ya Posta Afrika.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), akihutubia Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU, makao makuu ya umoja huo jijini Arusha, leo Juni 11,2024.

Msimamo huo wa Serikali umetolewa leo Juni 11, 2024 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), wakati akihutubia Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU, unaofanyika makao makuu ya umoja huo jijini Arusha.

"Kwa heshima kubwa, napenda kuthibitisha msimamo usioyumba wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusaidia mipango mbalimbali ya PAPU," amesema Mhandisi Mahundi aliyekuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.

Mhandisi Mahundi ameutaka mkutano huo wa PAPU, kutafakari njia zitakazowezesha mageuzi ya posta Afrika, ili kuendana na maendeleo ya kasi ya biashara mtandao (e-commerce), pamoja na mabadiliko makubwa ya teknolojia ya mawasiliano na dijitali.

Wajumbe wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyotolewa leo Juni 11, 2024 na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi. Mkutano huo, unaofanyika jijini Arusha.

Naibu Waziri huyo amesisitiza kwamba barani Afrika, posta inafanya kazi kubwa ya kutoa huduma za kuaminika, uhakika na zenye tija kwa biashara kubwa, ndogo na za kati (MSMEs).

“Ni vizuri kwamba wakati dirisha la biashara mtandao likiwa limefunguka na kuja na fursa zaidi, tayari baadhi ya Posta Afrika zimeanza kujishughulisha na kutoa huduma mbalimbali katika mnyororo wa biashara mtandao,” amesema Maryprisca Mahundi.

Amesema, bado kila mtu anakumbuka matukio ya Septemba 3 mwaka uliopita, liliposhuhudiwa tukio la kihistoria la uzinduzi wa Jengo la Makao Makuu ya Ofisi za PAPU jijini Arusha, uliofanywa na Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Katikati), akishuhudia tukio la Katibu Mkuu wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) Dk. Sifundo Chief Moyo (kushoto) kupokea kompyuta 60 na Kamera ya Video kwa ajili ya Kituo cha Umahiri cha Huduma za Posta Kidijitali kutoka kwa wawakilishi wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) na Shirika la Posta Ufaransa.

Amebainisha kuwa tukio hilo la kihistoria la nembo hiyo ni kielelezo na uthibitisho wa uhakika wa uongozi wa dhati na wenye maono wa viongozi wa Tanzania kuhusu mikakati na malengo ya PAPU.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, uzinduzi wa PAPU Tower ni alama ya juhudi za pamoja za nchi wanachama wa umoja huo katika kuendeleza ugunduzi, kuimarisha mawasiliano na kukuza maendeleo katika eneo lote la Afrika.         

Mkutano huo wa Baraza la Utawala la PAPU, unatarajiwa kujadili maazimio na taarifa za vikao vya Kamati za Wataalam wa masuala ya posta vilivyoanza Juni 03 hadi 7, 2024, kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Fedha na Utawala, Sera na Kanuni, Uendeshaji na Teknolojia pamoja na Mikakati.

Wajumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi, iliyotolewa leo jijini Arusha, unapofanyika mkutano huo.

Awali, akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Nicholaus Merinyo Mkapa, amesema udhibiti madhubuti wa maafa na hatari ni muhimu katika ulimwengu wa leo, hivyo Sekta ya Posta lazima iwe thabiti na tayari kukabiliana na majanga ya asili, vitisho vya mtandao na hatari zingine.

Mkapa amesema  hatua hiyo inahusisha kuandaa mipango ya kina ya udhibiti wa maafa na hatari, kuwekeza katika miundombinu salama na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ili kushughulikia dharura kwa ufanisi.

Amesema mfumo thabiti wa Sera ya Posta ni muhimu kwa ajili ya kuongoza sera za mahitaji ya sekta zinazokuza uvumbuzi, ushindani na maendeleo.

Nauli Dar-Dodoma treni ya mwendokasi Sh 31,000

  -Kuumiza kichwa wenye mabasi

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeutangazia umma wa Watanzania nauli  kwa safari ya treni za Mwendokasi, maarufu SGR, kuwa ni Sh 69.51 kwa kilomita,huku watoto kuanzia kuanzia miaka 4 hadi 12 wakitakiwa kulipia Sh34.76 kwa kilomita.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwaaga viongozi wa dini 104 waliokuwa wakielekea Dodoma kwa Treni ya Mwendokasi (SGR), Jumatatu, Aprili 22, 2024. Picha ya Mtandao.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nauli kwa safari ya Dar es Salaam hadi Dodoma iliyo na umbali wa kilometa 444.0 itakuwa Sh31,000, huku safari ya Dar hadi Moro ya umbali wa kilometa 192.0 ikiwa Sh13,000 kwa watu wazima.

Nauli za watoto kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma itakuwa Sh15,500 na kwa safari za Dar kwenda Moro ni Sh 6,500 huku ikielezwa watoto mwenye umri chini ya miaka minne (4) hawatalipa nauli.

Nauli hizo za Treni ya Mwendokasi (SGR), zinaelezwa kuwa zitaongeza tija kwa uchumi wa taifa kutokana na kutumia muda mfupi kwa safari zake, ambapo kutoka Dar hadi Moro itatumia muda wa saa 2, huku Dar hadi Dodoma ikiwa na uwezo wa kutumia saa 4.

Muda huo wa safari unakadiriwa kuwa nusu ya ule unaotumiwa na mabasi ya abiria kutoka Dar kwenda Moro ambayo kwa kawaida hutumia saa 3.30 hadi 4 huku ya Dodoma yakitumia saa8 hadi 9.

Si hivyo tu, bali nauli za mabasi zinakaribiana na treni, huku baadhi ya mabasi ya madaraja ya kati na VIP yakitoza nauli zaidi ya zile za Treni ya SGR, ambazo ni kati ya Sh29,000 na Sh45,000.

Hali hiyo huenda ikaibua changamoto mpya kwa wamiliki wa mabasi ya abiria yanayofanya safari kwa njia hizo, kutokana na ukweli kwamba, nauli za treni za SGR na muda mfupi wa safari kwa treni hizo, utawavutia zaidi wasafiri, wakipungua kutumia mabasi.

Nauli hizo za SGR zinatajwa ni kwa baraka ya Bodi ya Wakurugenzi ya LATRA, uliotokana na kufanyia kazi maombi yaliyoletwa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), taarifa zilizopokelewa kutoka TRC na wadau wengine. 

Soma taarifa kamili ya LATRA hapa chini:





RC Nawanda 'aliwa kichwa' mchana kweupe

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda, 'ameliwa kichwa' mchana kweupe. Ndivyo unavyoweza kueleza baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 11, 2024, huku Kenan Kihongosi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, akiteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa huo.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

Kutenguliwa kwa uteuzi wa Nawanda, kumeandamana na maelezo, pia tuhuma mbalimbali zilizozagaa mitandaoni zikimtaja kwa jina kiongozi huyo kudaiwa kuhusika nazo, maeneo mbalimbali alipohudumu kama kiongozi.

Dk. Yahya Nawanda

Taarifa ya Ikulu, iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, imeleeza kuwa mbali na Rais Samia kutengua uteuzi wa Dk. Nawanda na kuteua mbadala wake, pia amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya  Momba ambaye sasa ni Elias Mwandobo akichukua nafasi ya Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Kabla ya uteuzi huo, Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Ikulu.

Zaidi soma taarifa ya Ikulu hapa chini;


Jumatatu, 10 Juni 2024

Naibu Waziri Mahundi kufungua Baraza la 42 PAPU kesho

Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha 

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Juni 11, 2024 Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo jijini Arusha.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb).

Mkutano huo utakaofanyika kwa siku 2 kuanzia  Juni 11 hadi 12,unatarajiwa kujadili maazimio na taarifa za vikao vya Kamati za Wataalam wa Masuala ya Posta vilivyoanza jijini humo Juni 03, 2024, ambavyo vilijadili masuala mbalimbali yanayohusu fedha na utawala, mikakati, sera na kanuni pamoja na uendeshaji na teknolojia.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 45 wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Posta kutoka barani Afrika na wajumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Posta Duniani.

Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya Sekta ya Posta Afrika likiwa na jukumu la kuziunganisha nchi wanachama katika kupata fursa, kujadili changamoto na kutafuta suluhu endelevu kwa ajili ya kuboresha huduma za posta katika mataifa 45 wanachama.

Wajumbe wa vikao vya Kamati za Wataalam wa Masuala ya Posta vilivyoanza jijini Arusha Juni 03,2024 kujadili masuala mbalimbali ikiwamo fedha na utawala, mikakati, sera na kanuni pamoja na uendeshaji na teknolojia, wakifuatilia vikao hivyo kuelekea mkutano unaofunguliwa leo na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi. 

Ijumaa, 7 Juni 2024

Wafanyabiashara wa ng'ombe wamuunga mkono Rais Samia

-Kufanya maonyesho Juni 14 Chalinze

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com 

CHAMA cha Wafanyabiashra wa Ng'ombe Tanzania (TCCS), kimesema kinaendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha sekta ufugaji nchini inazidi kuboreshwa kufikia ufugaji wa kisasa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kibiashara wa Ng'ombe(TCCS), Naweed Mulla (aliyevaa kofia),wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya mifugo na mnada, unaotarajiwa kufanyika Juni 14 -15, 2024 maeneo ya Ubena Estate Chalinze.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji wa Kibiashara wa Ng'ombe nchini (TCCS), Naweed Mulla ameeleza hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu maonesho ya mifugo na mnada unaotarajiwa kufanyika Juni 14 -15, 2024 maeneo ya Ubena Estate Chalinze.

"Lengo la kuanzisha programu hizo ni kusaidia wakulima na wafugaji kujikwamua kiuchumi wao wenyewe na kuongeza  Pato la Taifa kupitia ufugaji," amesema Mulla.

Amebainisha kuwa takribani washiriki 300 wanatarajiwa kushiriki maonesho hayo yatakayofanyika kwa siku tatu, huku akitoa wito kwa vijana na wafugaji wapya wanaotamani kuingia katika shughuli za ufugaji kushiriki katika maonesho hayo, ili waweze kujifunza mambo mbalimbali ya ufugaji na kuona namna watakavyoweza kufanya biashara hizo za kilimo.

Mulla amesema maonesho hayo yana nia ya kuwezesha Jukwaa Madhubuti la Kitaifa la Wafugaji, wasindikaji na wadau katika mnyororo wa thamani ya mifugo, kutambulika kwa lengo la kuendeleza sekta hiyo kwa mbinu bora, endelevu za kiuchumi na kimazingira.

''Tamasha hilo lilianzishwa na kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2022, ambapo kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyiwa maboresho makubwa yatakayoenda sanjari na utoaji wa elimu, ili kutoa msaada kwa jamii namna ya kufuga kwa tija,''amesema Mulla na kuongeza;

''Tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora, rafiki na wezeshi kuhakikisha sekta ya mifugo inawakwamua wakulima na wafugaji kimaisha na kuhakikisha wanaongeza tija na ubunifu katika shughuli za kilimo.''

Naye Kaimu Mkurugezi Idara ya Mipango, Ushauri na Uhusiano wa Benki ya Kilimo, Mkani Waziri amesema kazi yao kubwa ni kusaidia sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi vinapata maendeleo, hivyo wameamua kushirikiana na TCCS kuona namna wanavyoweza kuleta mageuzi katika tasnia ya ufugaji.

Amesema Benki ya kilimo wamekuwa washiriki wakuu katika sekta ya ufugaji ili kuhakikisha  Watanzania wanafuga kwa tija na kuweza  kupata kipato cha  kuboresha maisha yao.

''Tunatoa  mikopo ya moja kwa moja kwa wafugaji katika kuwawezesha wafugaji na hadi sasa benki imetoa jumla ya Sh.bilioni 38 ya mikopo kwa wafugaji  kwa wanufaika wapatao 8688 katika mikoa 21,''amesema na kuongeza;

''Tumekuwa tunashirikiana na taasisi nyingine za fedha katika kuchangiza  taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwa kutoa dhamana ya asilimia 50 hadi 70 kwa mikopo mfugaji anaochukua lengo ikiwa ni kuwainua wafugaji wakitanzania,''alisema.

 Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Mkoani Pwani, Ngobere Msamau amesema kupitia maonesho hayo wanatarajia kupata  elimu ya kufanya wazidi kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa na kuondokana na ule wa kienyeji.


Wafungisha ndoa wapewa siku 4 kujisajili e-RITA

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

KABIDHI Wasii Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Frank Kanyusi amewataka wafungishaji ndoa wote nchini kuhakikisha wamejisajili  kwenye mfumo wa kidijitali wa e-RITA ifikapo Juni 10, 2024.

Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Bw Frank Kanyusi  akisisitiza jambo kwa Waandishi wa habari  kuhusu umuhimu kwa wafungishaji ndoa wote nchini kujisajili kwenye mfumo wa kidijitali wa e-RITA.

Agizo hilo hilo limetolewa na Kabidhi Wasii Mkuu Juni 6,2024, Dar es Salaam, ikiwa ni siku nne, kabla ya siku ya mwisho kujisajili, sawa na saa 96 za utekelezaji kwa walengwa.

“Mfumo huu wa kidijitali utawazeshesha wahusika kutambulika katika kanzidata ya Msajili Mkuu wa Ndoa na Talaka, pia kupata leseni mpya za kidijitali za kufungisha ndoa,” amesema Kanyusi na kuongeza; "Mfumo huo utaongeza ufanisi na kuongeza udhibiti wa usajili wa ndoa."

Kanyusi amewataja walengwa katika zoezi hilo kuwa ni wafungishaji ndoa wote kutoka dini na madhehebu yote nchini, akibainisha kwamba usajili wa kundi hilo siyo utaratibu mpya bali umekuwa ukifanyika kwa miaka mingi kupitia mfumo wa analojia.

“Kuanzia Januari mwaka huu mpaka sasa tayari wafungishaji ndoa 3,635 wameshajisajili kwenye mfumo wa e-RITA. Natoa rai kwa wale ambao hawajajisajili kwenye mfumo, kufanya hivyo kwani shahada za ndoa zitatolewa kwa wale waliosajiliwa tu kwenye mfumo,” amesisitiza Kanyusi.

Kwa mujibu wa Kabidhi Wasii Mkuu huyo, zoezi hilo la usijili  linawahusu wafungishaji wote hata wale ambao walishasajiliwa awali  kwenye mfumo wa anajojia, ikijumuisha walio na leseni hai na ambao leseni zao zimekwisha muda wake, hivyo kuhitaji kuhuishwa.

Amebainisha kwamba kuanzia sasa wafungishaji ndoa wapya watatakiwa kutumia mfumo mpya  wa kidijitali wa e-RITA na kupata leseni zinazowapa mamalaka kisheria ya kufunga ndoa.

“Ili kujisajili wafungishaji ndoa wanatakiwa kuingia kwenye tovuti ya Wakala yaani www.rita.go.tz kisha bofya kitife kilichoandikwa e-RITA na kuchagua huduma ya Ndoa na Talaka baada ya hapo utapata maelekezo,” amesema.

Akifafanua zaidi, Kanyusi amesema zoezi la usajili linahusisha ujazaji wa taarifa binafsi za mfungishaji ndoa, dini na dhehebu lake na pia atahitaji kuthibitishwa  na viongozi wa dhehebu lake.

“RITA imeendelea kufanya maboresho katika utoaji wa huduma zake kwa njia ya kielekroniki kwa lengo la kuongeza ufanisi sambamba na kusogeza huduma zake karibu na wananchi pamoja kufikia matarajio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,” ameongeza.


Alhamisi, 6 Juni 2024

Hamad Rashid kuachia kiti ADC, Doyo akiwania

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democrac Change (ADC) Taifa, Doyo Hassan Doyo ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa  wa chama hicho, baada ya

Katibu Mkuu wa Chama Cha Alliance for Democrac Change (ADC) Taifa, Doyo Hassan Doyo (Katikati) akitangaza nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Taifa  wa chama hicho mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam, Juni 6, 2024.

mwenyekiti wa sasa Hamad Rashid Mohamed kumaliza muda wake kikatiba.

Akitangaza nia yake leo Juni 6, 2024 jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari, amesema ameona kuwa anaamimi ana uwezo wa kukitumikia chama hicho katika kutekeleza matakwa ya Katiba.

"Kutokana na uzoefu wa miaka 10 nilioupata kutoka kwa Mwenyekiti aliiyemaliza muda wake naahidi kuyaendeleza mazuri yote hususani kuilinda Katiba ya chama.

"Mwenyekiti Hamad ametufunza jambo katika chama kwani ameonyesha kufuata matakwa ya Katiba kwa kuachia ngazi baada ya kumaliza muda wake na kuwapa funzo vijana wa chama hicho na wanasiasa wengine nchini wanaong'ang'ania madaraka," amesema Doyo.

Amebainisha kuwa, Juni 11 mwaka huu atachukua fomu rasmi kwa ajili ya kugombea nafasi hiyo na kuwaomba wanachama wenzake ndani ya chama itakapofika Juni 27 mwaka huku wamchague Ili aweze kufanya yote aliyokusudia na chama kiweze kufikia viwango vya juu. 

Ameongeza kuwa, endapo atafanikiwa kushinda nafasi hiyo atakisaidia chama kusukuma ajenda za upatikanaji wa ajira, elimu Bora,na kupata wabunge wawakilishi watakaowakilisha wananchi katikà changamoto zao bungeni.

Naye Mwenyekiti wa Vijana Taifa wa ADC, Ibrahimu Pogora amempongeza Doyo kwa kutangaza nia yake na kuahidi kushirikiana naye katikà harakati zote za uchaguzi, kupata wadhamini Bara na visiwani.

Amewataka wanachama wa chama hicho kutambua kuwa wanadhamana na mtia Nia wa nafasi hiyo kwa kuwa Doyo si mwanachama wa kuletwa  bali ni mwanzilishi wa chama hicho

Wakati huo huo, Scola Kahana aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Kibaha Mjini mwaka 2020 kupitia chama hicho ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Taifa Ili aweze kushirikiana na Mwenyekiti Taifa kukinoa chama hicho na kukiwezesha kuwa chama cha mfano.


Majengo, eneo Urafiki yauzwa kwa NHC

-NHC yalipa mabilioni: Ni kupitia mnada wa wazi,  

-Thamani ya NHC kuongezeka: Sasa kuboresha mandhari


Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limenunua rasmi eneo la Urafiki na majengo yaliyokuwa chini ya Kampuni ya Urafiki wa Tanzania na China (Tanzania - China Friendship Textile CO LTD). 

Sehemu ya majengo ya kilichokuwa la Kiwanda cha Urafiki, ambayo sasa yanamilikiwa na NHC.

Hatua hiyo, itaongeza ukubwa wa mtaji na thamani ya shirika hilo la nyumba, linalotajwa kuongoza kwa ukubwa wa mtaji na uwekezaji barani Afrika, huku NHC likitajwa pia kuidhinisha na kusaini mikataba ya miradi 21 ya ubia yenye thamani ya Sh.bilioni 271  kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya ameyasema hayo leo wakati wa ziara ya kukagua maeneo mbalimbali, ambayo sasa yatakuwa chini ya miliki ya NHC na kufafanua kuwa eneo hilo linajumuisha nyumba, maghala, viwanja vya wazi, viwanda na mali nyinginezo.

Habari zaidi za ndani kutoka vyanzo vingine, zinaonyesha kwamba mashine na mitambo ya kilichokuwa Kiwanda cha Nguo Urafiki, vimeuzwa kwa watu tofauti na NHC kwa njia ya mnada, kutumia mtindo wa mafungu. (LOT).

Katika ziara yake, Saguya ameelezea furaha yake na matumaini makubwa kuhusu hatua hiyo, akibainisha kwamba itasaidia kuboresha miundombinu na kuinua uchumi wa maeneo hayo ikiwamo kuboresha mandhari ya Dar es Salaam.

Mbali na kununua majengo hayo, NHC inaendelea kufanya ukarabati katika majengo yake 181 yenye vyumba 3,111 yaliyo katika mikoa mbalimbali nchini, huku ujeni wa nyumba 560 awamu ya kwanza eneo la Kawe Dar es Salaam ukiwa umefikia asilimia 60 na ujenzi wa jengo la Morocco Square ukikamilika na upangishaji hoteli ukifanyika kwa asilimia 100, maduka asilimia 94 na ofisi asilima 39..

Amesema kuwa NHC, imelinunua eneo hilo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 50 kutoka kwa mnada wa wazi kikiwa na thamani ya mabilioni ya fedha.

Mkurugenzi wa NHC (Wa kwanza kulia) akionyeshwa  sehemu ya eneo lililokuwa na Kiwanda cha Nguo Urafiki, Ubungo Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa Shirika la Nyumba la Taifa, Muungano Saguya.

Amesema:"Kupitia umiliki huu mpya, Shirika la Nyumba la Taifa limejipanga kuboresha maeneo haya ili kuendana na malengo yetu ya kutoa makazi bora na ya kisasa kwa wananchi. Tumeanza kwa kulipima eneo lote na kutambua mipaka yote inayohusisha eneo hilo."

Kwa mujibu wa Saguya, eneo la Urafiki lina historia ndefu ya kuwa kituo muhimu cha viwanda na makazi, kikitoa mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania. 

"Hivi sasa, NHC inapanga kufanyia maboresho makubwa eneo hili kwa kujenga miundombinu bora, nyumba za kisasa na maeneo ya biashara ambayo yatavutia wawekezaji na wakazi wapya, "amesema Saguya.

Ameongeza: "Shirika la Nyumba la Taifa linaamini kuwa mradi huu mpya utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa kwa ujumla na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya makazi na maendeleo ya kiuchumi nchini. Katika mpango wa maendeleo ya NHC, eneo la Urafiki litawekewa mkazo maalum kwa ajili ya kuhakikisha kuwa linakuwa mfano bora wa maendeleo ya kisasa na endelevu."

Baadhi ya maghala ya kilichokuwa Kiwanda cha Nguo Urafiki ambayo sasa ni mali ya NHC.Picha zote kwa hisani ya NHC.

Saguya alihitimisha kwa kusema, "Hii ni hatua muhimu kwa NHC na kwa taifa letu. Tunawaomba wananchi na wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi zetu katika kuboresha na kuendeleza maeneo haya kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wakati hayo yakiendelea, shirika hilo linaelezwa kukusanya Sh. bilioni 208.1 ambazo ni sawa na asilimia 76.1 ya lengo katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Wabia wakuu wa kiwanda hicho ni Msajili wa Hazina na Kampuni ya Urafiki wa Tanzania na China (Tanzania - China Friendship Textile CO LTD). Kiwanda hicho ni matokeo ya urafiki wa China na Tanzania na kina historia ndefu na uhusiano wa muda mrefu.

Awali, kulikuwa na mvutano mkubwa baina ya kampuni iliyokuwa inamiliki kiwanda hicho na wafanyakazi, jambo lililokuwa limewafikisha katika hatua mbalimbali za usuluhishi hadi kiwanda hicho kilipopigwa mnada ili kuweza kuokoa mali za Kampuni.

Hayo yalibainishwa wakati Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC), Hamad Abdallah, alipofanya ziara kutembelea miradi inayotekelezwa na NHC mkoani Dar es Salaam, kukagua na kuona maendeleo. 

Hamad amefanya ziara katika miradi ya Samia Housing, Morocco Square, Shule ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na  eneo la Urafiki  Dar es Salaam hivi karibuni.

HESLB: 'Elimu ya Juu sasa njooni mkope'

 Sh bilioni 787 zasubiri wanafunzi 250,000

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com 

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB), imetangaza kufunguliwa dirisha la kuomba mkopo kwa wanafunzi katika mwaka wa masomo 2024/2025, huku waombaji wakitakiwa kusoma mwongozo uliopo kabla ya kuomba mkopo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 6, 2024 Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Dk. Bill Kiwia,(pichani juu), amesema baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kuzindua miongozo Mei 27, 2024, waliiweka miongozo hiyo kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo ambayo ni; Www.heslb.go tz.

"Kwa mwaka wa masomo 2024/2025 dirisha la kuomba mkopo kwa njia ya mtandao lipo wazi kwa siku 90, kuanzia Juni 1 hadi Agosti 31, 2024," amesema Dk Kiwia.

Hata hivyo, Dk. Kiwia amesema muda wa siku tisini unatosha kwa waombaji na wanatakiwa kuandaa nyaraka muhimu, na itachukua dakika 40 kukamilisha maombi yake kwa njia ya Mtandao.

"Tunasisitiza waombaji kuzingatia muda uliotolewa kwa kuwa hatutarajii kuongezwa baada ya Agosti 31, 2024," amesema.

Amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga Sh. Bilioni 787 kwa ajili ya mikopo na ruzuku kwa jumla ya wanafunzi 250,000 ambapo idadi hiyo imeongezeka kutoka wanafunzi 224,056 mwaka 2023/2024 ambapo ni ongezeko la jumla wanafunzi 25,944.

Taka za plastiki zawapeleka wanafunzi Ustawi 'Hult Prize' Kenya

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Wanafunzi watatu kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii ni miongoni mwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali duniani wanaokutana jijini Nairobi nchini Kenya na kuchuana kuwania Tuzo ya 'Hult' kupitia mawazo yao ya kibiashara na ubunifu.

Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dk. Joyce Nyoni, (wa tatu kushoto), akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho watakaoshiriki kuwania tuzo ya Hult Prize jijini Nairobi, linaloendeshwa kwa ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa(UN), na timu za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani. Wengine pichani ni wanafunzi kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii, watakaoshiriki kuwania tuzo hiyo mwaka huu 2024.

 Wanafunzi hao kutoka Tanzania ni pamoja na Hellena Sailas,  Maria Daudi, na Method Dallu ambao wamechaguliwa kuwania tuzo hiyo kupitia wazo lao la kibishara na ubunifu linalohusu utengenezaji na uzalishaji wa matofali kwa kutumia taka za plastiki.

Tuzo ya Hult Prize ni shindano kubwa zaidi la ujasiriamali wa kijamii kwa wanafunzi duniani, linaloendeshwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa(UN), na timu za wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani. 

Akizungumza na wanafunzi hao ambao wamewasili jijini Nairobi jana, Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Dk. Joyce Nyoni amewapongeza kwa ubunifu huo na kuwatakia kila la kheri katika ushiriki wao.

Wanafunzi kutoka Chuo cha Ustawi wa Jamii Tanzania,Method Dallu, Hellena Sailas na Maria Daudi waliochaguliwa kuwania tuzo za Hult Prize kwa mwaka 2024 jijini Nairobi, kupitia wazo lao la kibishara na ubunifu la utengenezaji na uzalishaji wa matofali kwa kutumia taka za plastiki wakiwa eneo la kuhifadhia malighafi za utekelezaji mradi wao.

Mashindano hayo yanalenga kutatua matatizo ya kijamii kwa kuanzisha biashara ya kijamii inayoweza kukua na kudumu.

Washindi katika shindano hilo watawasilisha miradi yao mbele ya jopo la majaji mashuhuri, viongozi wa biashara duniani, viongozi wa mawazo na watetezi wa mabadiliko ili kushinda dola milioni moja za Marekani na kuanzisha biashara zao. 

Msimamo wa Tanzania PAPU huu hapa

Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha

Wakati vikao vya Kamati za Ufundi vya Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), vikiendelea kwa siku ya tatu  jijini Arusha, Tanzania imetoa msimamo wake baada ya kuwasilisha hoja zake ikiwemo inayopendekeza kuwa na mwakilishi kiongozi katika nafasi ya juu ya uongozi wa umoja huo.

Baadhi ya wawakilishi wa Tanzania kwenye mkutano wa Kamati za Ufundi vya Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), vinavyoendelea kwa siku ya tatu  jijini Arusha.

Wawakilishi wa Tanzania wametoa msimamo huo wakizingatia kwamba kwa mujibu wa mkataba wa PAPU, nchi mwenyeji ambayo kwa sasa ni Tanzania inalazimika kuchangia asilimia 50 ya bajeti ya uendeshaji ya umoja huo kila mwanzo wa mwaka wa fedha, iwapo nchi wanachama hazijachangia kwa wakati, fedha ambazo baadaye hurejeshwa.

"Katika hoja zetu, tumesisitiza Tanzania kupatiwa nafasi hiyo ili kuhakikisha usimamizi imara wa fedha zinazotolewa, ambazo Tanzania imekuwa ikilipa kama nchi mwenyeji, pia kusimamia kikamilifu, ili kupata marejesho ya gharama za ujenzi tulizolipa zaidi ya kiwango cha umiliki cha asilimia 40 kilichowekwa," alisema mmoja wa wawakilishi wa Tanzania katika mkutano hu, akioomba jina lihifadhiwe kwa kuwa sio msemaji.

Wawakilishi hao wa Tanzania wametoa pendekezo hilo la kuwa na mwakilishi kwenye nafasi ya juu ya uongozi wa PAPU, Juni 5, 2024  mbele ya Kamati ya Fedha na Utawala katika  vikao vya Wataalam wa Masuala ya Posta vinavyoshirikisha wajumbe kutoka mataifa 46 wanachama wa  PAPU.

Wawakilishi wa mataifa mbalimbali wakifuatilia mkutano wa Kamati za Ufundi vya Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), vinavyoendelea kwa siku ya tatu  jijini Arusha, Juni 5,2024. 

Katika hatua nyingine, kwenye Kamati ya Mkakati , wajumbe wa Tanzania walibainisha  mchango mkubwa wa Tanzania katika ujenzi wa jengo la PAPU lililopo jijini Arusha, ambapo mwaka huu 2024 unafanyika Mkutano wa 42 wa Baraza la Umoja wa Posta Afrika. 

Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo imeazimia  kuunda Kikosi Kazi katika Kamati ya Mkakati, kitakachoshughulikia upanuzi na ushirikishaji watoa huduma katika Sekta ya Posta, ambapo Tanzania imejitolea kushiriki pamoja na nchi za Botswana, Burkina Faso, Cameroon, DRC, Ivory Coast, Kenya, Misri, Namibia, Niger na Uganda.

Wajumbe hao pia wamejadili masuala ya mapato na matumizi ya umoja, miradi, ajira na stahiki za watumishi wazawa, michango ya ada za uanachama na Mpango Mkakati wa miaka minne wa sekta ya posta barani Afrika, ili iweze kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Jumatano, 5 Juni 2024

EWURA yaweka hadharani bei mpya ya petroli

-Dar sasa bei  Sh3,261, Dodoma Sh3,320, Bukoba Sh3,476


Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com

Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo  ya mafuta ya petroli na bidhaa zake nchini kwa mwezi Juni, huku ikiainisha bei ya chini kuwa ni Sh 3,261 kwa lita moja ya petroli Dar es Salaam na bei ya juu ni Sh 3,476 mkoani Kagera.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Mwainyukule

Kwa mujibu wa EWURA, bei ya lita moja ya diseli kwa Dar es Salaam ni Sh3,112 huku wilayani Tanganyika ikiwa Sh 3,288 kwa lita moja na mafuta ya taa yakiwa bei sawa na petroli kwa maeneo hayo.

Taarifa ya EWURA iliyotolewa Juni 5, 2024 kupitia mkurugenzi wake mkuu, Dk. James Mwainyukule, imeeleza kuwa bei kikomo za rejareja kwa lita moja ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ni Sh 3,261 huku kwa Bandari ya Tanga ikiwa Sh3,263 kwa lita.

Katika jiji la Dodoma bei ya lita moja ya petroli ikiwa Sh3,320, dizeli Sh3,171 na mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh3,319 kwa lita, huku jijini Arusha, bei ya lita moja ya petroli ni Sh3,320,  dizeli Sh 3,178 na mafuta ya taa ni Sh3,345.

Katika jiji la Mwanza, bei ya lita moja ya petroli ni Sh 3,411 petroli, Sh3,262 dizeli na mafuta ya taa Sh 3,411.

Zaidi soma jedwali la bei mpya ya mafuta iliyotolewa na EWURA Juni 5, 2024





Jumatatu, 3 Juni 2024

'Wataalam Posta tumieni maendeleo teknolojia kufungua fursa za kiuchumi'

 MWANDISHI WETU, WHMTH, Arusha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar, Dk. Mzee Suleiman Mndewa, amewataka wataalamu wa masuala ya Posta Afrika, kutumia vyema maendeleo ya teknolojia katika kuwezesha sekta hiyo kufungua fursa za kiuchumi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi katika nchi hizo.

Washiriki wa vikao vya Kamati za Wataalamu wa Masuala ya Posta kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU0, uliofanyika jijini  Arusha, Juni 3, 2024. vikao hivyo ni vya utangulizi kabla ya Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU litakalofanyika Juni 11 hadi 12 jijini humo. 

Dk. Mndewa amesema hayo Juni 03, 2024 mkoani Arusha wakati akifungua Vikao vya Kamati za wataalamu wa masuala ya posta kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), ikiwa ni vikao vya utangulizi kabla ya Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la PAPU litakalofanyika Juni 11 hadi 12 jijini humo.

Amesema kuwa ili nchi za Afrika ziweze kufanikiwa zaidi katika masuala ya Posta na kuendana na kasi ya ukuaji wa Biashara Mtandao, nchi wanachama kwa pamoja zina wajibu wa kuhakikisha kila mmoja anashiriki katika uchumi wa kidigitali. 

"Ni wajibu wetu kuhakikisha tunatafuta ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili nchi wanachama, kwani  bado kuna changamoto kwenye nchi za Afrika, ikiwemo miundombinu na teknolojia, zinazohitaji  kupatiwa ufumbuzi ili kurahisisha mawasiliano kwa haraka," amesema Dk.Mndewa. 

Amebainisha kuwa ni vema nchi za Afrika kwa umoja wao zikahakikisha zinatumia teknolojia ili kupunguza gharama na kutimiza malengo ya nchi waliyojiwekea ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya teknolojia yanayoshuhudiwa kote duniani.

Naye Katibu Mkuu wa PAPU, Dk. Sifundo Chifu Moyo amesema, zipo changamoto kadhaa zinazokabili sekta ya Posta zinazowafanya wateja kutokuwa na furaha, lakini kwa sasa kwa asilimia kubwa viongozi wa nchi hizo wameanza kuzitafutia ufumbuzi.

Ametaja moja ya changamoto kuwa ni kutikisika kwa Mauzo ya Hisa katika Soko na kushuka kwa mapato hivyo, vikao vya kamati hizo  za wataalamu, vinatarajiwa kutoa majawabu ya namna teknolojia inavyoweza kuwa suluhu ya changamoto hizo ili kurejesha imani ya wananchi katika sekta hiyo.

“Kama wote mnavyoelewa, teknolojia haimilikiwi na mtu yeyote. Kwa hiyo kila mmoja ana fursa ya kuitumia vizuri teknolojia ili kujikwamua kiuchumi na sekta ya Posta haipaswi kuwa nyuma. Kwa sasa Posta inaichukulia teknolojia kwa uzito mkubwa na ipo kwenye sera zake, pia inahakikisha teknolojia inapelekwa karibu zaidi na wananchi,” amesema Dk. Moyo.

Amesema ana furaha kwa kuwa baada ya miaka arobaini kwa mara ya kwanza mkutano huo unafanyika katika jengo la PAPU, ambalo ni moja ya vitega uchumi na kielelezo cha uwepo wa PAPU ambalo litadumu kwa miaka mingi ijayo kuonyesha uhai wa sekta ya Posta.