Takukuru yakunjua makucha Kigoma

-Wakandarasi ' watemeshwa bungo' Mwandishi Wetu,Kigoma Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Kigoma (TAKUKURU) imebaini upungufu mkubwa katika miradi 33 yenye thamani ya shiligi bilioni 12.5, iliyoifuatilia, ikionyesha kuwa chini ya kiwango. Kufuatia uchunguzi huo, wazabuni wawili waliobanwa na Takukuru, mmoja amerudisha fedha zadi ya shilingi milioni 125 na mwingine kuwasilisha mabati mapya kwenye mradi. Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Mkoa Kigoma, Leonida Mushama amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji ya taasisi Takukuru mkoani humo kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba mwaka huu. Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma Mkoa Kigoma, Leonida Mushama akiwasilisha taarifa ya Takukuru mkoani humo. Alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya Mkuu wa TAKUKURU mkoa Kigoma, Stephen Mafipa. Mushama amesema kuwa katika miradi hiyo pia ipo miradi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa mpango wa BOOST, yenye thamani ya takriban shilingi bilioni tatu. Amesema Takuk...