Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahya Nawanda, 'ameliwa kichwa' mchana kweupe. Ndivyo unavyoweza kueleza baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 11, 2024, huku Kenan Kihongosi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Momba, akiteuliwa kuwa mkuu mpya wa mkoa huo.
![]() |
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan |
Kutenguliwa kwa uteuzi wa Nawanda, kumeandamana na maelezo, pia tuhuma mbalimbali zilizozagaa mitandaoni zikimtaja kwa jina kiongozi huyo kudaiwa kuhusika nazo, maeneo mbalimbali alipohudumu kama kiongozi.
![]() |
Dk. Yahya Nawanda |
Taarifa ya Ikulu, iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga, imeleeza kuwa mbali na Rais Samia kutengua uteuzi wa Dk. Nawanda na kuteua mbadala wake, pia amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Momba ambaye sasa ni Elias Mwandobo akichukua nafasi ya Kihongosi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi huo, Mwandobo alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Ikulu.
Zaidi soma taarifa ya Ikulu hapa chini;
0 Maoni