Exuperius
Kachenje, daimatznews@gmail.com
Dar mpaka Moro, hayawi, hayawi, sasa yamekuwa. Tanzania inaandika historia mpya katika nyanja ya usafiri na usafirishaji Saa12 kamili ya Juni 14, 2024, ambapo Treni ya Mwendokasi (SGR) inayotumia umeme, ikianza safari zake kwa kubeba abiria kibiashara.
![]() |
Treni ya Umeme ya SGR |
Treni hiyo
itaanza safari zake, kabla ya muda uliopangwa wa Julai mwaka huu kufika, ambapo
itaanza kwa safari za Dar es Salaam kwenda Morogoro.
Nauli kwa abiria mmoja kwa kila safari ni Sh13,000 mtu mzima huku watoto wenye umri zaidi ya miaka minne wakitakiwa kulipa nusu ya nauli ya mtu mzima.
Daima Tanzania blog, ilikuwepo kwenye kituo kikuu cha treni hiyo maeneo ya Steshen", ambapo ilishuhudia maandalizi ya mwisho yakiendelea, huku wananchi waliojaa bashasha, wakiingia na kuulizia upatikanaji wa tiketi.
Hata hivyo, walielezwa kuwa wanaweza kupata titeki hizo kupitia mtandao wa TRC au wawahi kufika kituoni hapo kabla ya muda wa safari.
Ratiba
iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), inaonyesha kwamba treni ya kwanza
ya Dar mpaka Moro, itaanza safari saa 12 kamili asubuni ambapo itasafiri kwa
takriban dakika 109 kukamilisha safari yake.
Dakika hizo
109 ni sawa na saa 1 na dakika 49, ikimaanisha kwamba kwa mara ya kwanza abiria
wa SGR, watafikishwa mjini Morogoro saa 1 na dakika 49.
Treni ya
kwanza ya SGR kutoka Moro itaanza safari yake saa2:50 asubuhi na kuwasili Dar
saa 4:39, huku treni ya pili kwenda Moro ikitoka Dar saa10 kamili jioni na
itafika Moro saa 11:49.
Safari ya
nne na ya mwisho kila siku katika ratiba ya safari hizo, itakuwa ikianzaia Moro
kwenda dar, ambapo itaondoka saa 1:30 usiku na kuwasili Dar saa 3:19 usiku.
Kwa mujibu
wa TRC, safari za treni hiyo zitafanyika kila siku, kuanzia Jumatatu hadi Jumapili.
0 Maoni