Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Juni 11, 2024 Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo jijini Arusha.
![]() |
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb). |
Mkutano huo utakaofanyika kwa siku 2 kuanzia Juni 11 hadi 12,unatarajiwa kujadili maazimio na taarifa za vikao vya Kamati za Wataalam wa Masuala ya Posta vilivyoanza jijini humo Juni 03, 2024, ambavyo vilijadili masuala mbalimbali yanayohusu fedha na utawala, mikakati, sera na kanuni pamoja na uendeshaji na teknolojia.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 45 wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Posta kutoka barani Afrika na wajumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Posta Duniani.
Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya Sekta ya Posta Afrika likiwa na jukumu la kuziunganisha nchi wanachama katika kupata fursa, kujadili changamoto na kutafuta suluhu endelevu kwa ajili ya kuboresha huduma za posta katika mataifa 45 wanachama.
0 Maoni