Exuperius Kachenje, daimatznews@gmail.com
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amelifahamisha Bunge la Jamhuri ya Muungano kuwa msimu ujao Ligi Kuu Tanzania, itaanza kutumia VAR.
![]() |
Mashine ya VAR |
VAR ni mfumo wa usaidizi kwa waamuzi wanapochezesha soka uwanjani kutumia 'video'.
Dk. Nchemba ametoa maelezo hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2024/2025 bungeni, mjini Dodoma leo, ambapo amesema lengo la kutumia mfumo huo ni kuhakikisha matokeo yanayopatikana yanakuwa ya haki.
"Msimu ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania, tutaanza kutumia ''VAR'' ili kuhakikisha matokeo yanayopatikana uwanjani yanakuwa ya haki ,"amesema Dk.Mwigulu na kuongeza:
"Maana kuna timu zimezidi - msimu mmoja penati 10, halafu zikifungwa zenyewe magoli yanakataliwa."
Waziri wa Fedha, amesema kuwa ili kuwepo na ''VAR'' za kutosha katika viwanja vyote, anapendekeza Bunge litoe msamaha kwenye uingizaji wa mashine hizo na vifaa vyake.
"Ufafanuzi utakaotolewa hapo baadae, INAWEZEKANA," amesisitiza Dk. Mwigulu
Kuhusu ubora wa eneo la kuchezea kwenye viwanja mbalimbali, Dk. Mwigulu amesema tayari Serikali ilitunga sheria inayotoa msamaha kwenye uingizaji wa nyasi bandia na vifaa vyake.
0 Maoni