-Kutoka mchanga hadi mnara wa matumaini katikati ya Moro -NHC yawekeza bil 2.5, yapandisha hadhi Mji kasoro bahari -Ni jengo linalobadilisha sura ya Morogoro Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Hakika sasa Morogoro ni mjini kasoro bahari, kwani katikati ya mji huo uliobeba historia ya kusifika ya milima inayotiririsha maji, utawala wa Chifu Kingalu wa Waluguru, wasanii wakongwe wa muziki nchini hata chimbuko la vipaji vya mpira nchini imesimikw alama mpya ya matumaini na maendeleo. Ukitaja historia ya Morogoro, huwezi kuwaweka kando wasanii maarufu wa muziki kuwataja wachache kama marehemu Mbaraka Mwishehe na Moro Jazz, lakini pia huiweki kando Cuban Marimba Band na marehemu Juma Kilaza. Lakini kwa mpira wa miguu huwezi kuwaacha Gibson Sembuli (marehemu), Husein Ngulungu(marehemu), Hamisi Gaga(marehemu) na Zamoyoni Mogella, tukiwataja kwa uchahe. Jengo hilo linaloongeza thamani ya Morogogro linajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia Mradi wa 2H-Morogoro,...