Raila Odinga afariki dunia
Nairobi,Kenya.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, (Pichani chini),amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Chanzo kutoka ofisi ya Odinga, kimeliambia Shirika la Habari la Reuters Jumatano, bila kufafanua.
Awali, Gazeti la India la Mathrubhumi liliripoti kuwa Odinga, ambaye alikuwa akipata matibabu mjini Kochi, Kusini mwa India, alipatwa na shambulio la moyo Jumatano na alihamishiwa hospitalini ambapo baadae alitangazwa amefariki.
Enzi za uhai wake akiwa kiongozi wa upinzani, Odinga aligombea urais wa Kenya mara tano bila mafanikio, mbili kati ya hizo zilisababisha machafuko makubwa, umwagaji damu na malalamiko miaka kumi mfululizo.
Hata hivyo ushiriki wake katika harakati za kidemokrasia kwa miaka mingi, ziliisaidia kuimarisha mageuzi mawili makubwa nchini Kenya, moja likiwa demokrasia ya vyama vingi mwaka wa 1991 na pili ni Katiba Mpya nchini humo mwaka wa 2010.
Odinga aliongoza maandamano baada ya uchaguzi wa 2007 uliozua mzozo mkali wa kisiasa tangu uhuru, ambapo takriban watu 1,300 waliuawa na mamia ya maelfu kuhamishwa makwao kutokana na mapigano hayo.

Maoni
Chapisha Maoni