TEC yajitenga waraka feki, yatoa taarifa kwa umma

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Baraza la Maaskofu Katolini Tanzania (TEC), limekanusha kuhusika na waraka uliokuwa ukizagaa mitandaoni Oktoba 13,2025 ukilihusisha Baraza hilo na waraka usio wake na kusema hiyo ni tabia mbaya kutumia TEC na kutaka ikomeshwe.

Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima 

Taarifa ya TEC iliyotiwa saini na Katibu wake Mkuu, Padri Charles Kitima imeeleza kuwa waraka huo wenye Kichwa cha Habari; TAMKO LA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA (TEC) KUHUSU AMANI KWA TAIFA KUELEKEA SIKU YA UCHAGUZI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UTAKAOFANYIKA TAREHE 29 OKTOBA 2025. "SAUTI YA WATU SAUTI YA MUNGU"  ni 'Fake'.

Padri Kitima amesema wanawatangazia Waamini na Watanzania wote kwa ujumla kuwa waraka huo haukutolewa na  Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. “Baraza halihusiki na hayo maudhui yaliyomo kwenye andiko hilo,” amesema.

TEC kupitia taarifa yake kwa umma yenye kumbukumbu namba TEC/GEN/1/2025 iliyobeba kichwa cha habari; YAH WARAKA "FAKE" ULIOSAMBAZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII, imesema; "Tabia hii mbaya ya kutumia Taasisi ya Maaskofu kupitisha ujumbe zisizotokana na Baraza ikomeshwe. Tunawataka wenye tabia hiyo waache…”


 

 


Maoni