TEF: Tutamkumbuka marehemu Mbega kwa mchango wake kukuza tasnia
Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) linasikitika kufangaza kifo cha Mwanachama wake Daniele Mbega, kilichotokea leo Oktoba 10,2025 alfajiri katika Hospitali ya Temeke alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuzidiwa.
![]() |
Marehemu Daniel Mbega |
Taarifa ya TEF iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Deodatus Balile, imeeleza kuwa mwili wa Mbega ambaye atakubukwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza tasnia ya habari nchini, utaagwa kesho Hospitali ya Temeke, dar es Salaam, kabla ya kusafirishwa kwenda Chigwingwili, Kongwa mkoani Dodoma kwa mazishi.
Kwa taarifa zaidi soma taarifa ya TEF chini...
Maoni
Chapisha Maoni