Uhamiaji yatimua wawili nchini

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Idara ya Uhamiaji nchini imewafukuza nchini raia wawili wa kigeni, Mmarekani mmoja na Mjerumani mmoja, ikieleza hatua hiyo imetoka na wawili hao kukiuka masharti ya viza zao za matembezi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Anna Makakala

Taarifa iliyotolewa leo na Uhamiaji imewataja raia hao kuwa ni Dk. Brinkel Stefanie mwenye hati ya kusafiria ya Ujerumani na Catherine Janel Amquist Kinokfu, mwenye hati ya kusafiria ya Marekani.

Uhamiaji imewataka raia wote wa kigeni wanaoingia nchini kwa madhumuni mbalimbali, kuzingatia matakwa yanayoainishwa katika viza au vibali vyao kuingia nchini.


 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi