Makamu wa Rais ashiriki Misa kumuombea Nyerere
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango ameungana na viongozi, Waumini pamoja na wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu. Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Francisko wa Asizi, Mwanjelwa Mkoani Mbeya leo tarehe 14 Oktoba 2025.
Ibada hiyo imeongozwa na Akofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Mbeya Mhashamu Gervas Nyaisonga.
Viongozi wengine wa kitaifa walioshiriki adhimisho hilo ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson.





Maoni
Chapisha Maoni