NHC yazindua nyumba za kifahari Dar,Tanga, Tabora

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

 Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limezindua rasmi mauzo ya nyumba katika miradi mikubwa ya kisasa jijini Dar es Salaam na mikoa ya Tanga na Tabora.


Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya NHC, Kambarage House, ukiongozwa na Meneja Mauzo na Masoko, Deogratius Batakanwa(pichani juu), ambaye amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora, ya kisasa na yenye thamani ya kudumu.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam, NHC imezindua Boulevard Residence yenye nyumba za chumba kimoja (37.7 sqm), vyumba viwili (103.5 sqm) na vyumba vitatu (124.2 sqm). 

Upo pia mradi wa Samia Housing Kijichi Residence ulio na nyumba za chumba kimoja (32.02 sqm), vyumba viwili (62.70 sqm) na vyumba vitatu (95.30 sqm).

Kwa Mkoa wa Tanga, NHC inatangaza mauzo ya nyumba kwenye mradi wake wa Mkwakwani Plaza wenye nyumba za vyumba viwili (80 sqm) na vitatu (108 sqm), huku mkoani Tabora ikijenga Tabora Plaza yenye vyumba viwili (95 sqm) na vitatu (124 sqm).

Bei za nyumba hizo zimepangwa kwa kuzingatia mahitaji ya Watanzania wa kipato tofauti, lengo kuu likiwa ni kutoa fursa kwa kila mmoja kumiliki nyumba bora. 

Kwa mujibu wa NHC, wateja wanaweza kupata huduma kwa kupiga simu kwenda namba ya huduma 0736 114 433 au kuwasiliana moja kwa moja na maofisa mauzo walioteuliwa.

Batakanwa amesema NHC itaendelea kujenga taifa kwa kuwapatia wananchi wa Tanzania makazi bora. 

Amewataka Watanzania kutumia fursa hiyo ya kipekee ya kumiliki nyumba katika maeneo yenye miundombinu bora na mazingira salama. 


Kupitia miradi hiyo, NHC imeonesha dhamira ya dhati, kuharakisha maendeleo ya makazi nchini na kuwapa wananchi fursa ya kuishi na kufanya biashara katika mazingira ya kisasa.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi