Mkurugenzi Mkuu NHC alivyocheza nambari nane, tisa mikoani

-Ni miezi minane tangu kuteuliwa -Atembelea mikoa tisa ya NHC Mwandishi Wetu, Bukoba Kwa wafuatiliaji wa mchezo wa mpira wa miguu yaani soka, anaelewa umuhimu wa namba nane na tisa kwenye mchezo huo, kwani anayecheza namba nane ndiye kiungo anayesukuma mpira kwa washambuliaji, huku namba tisa akisukuma mashambulizi na kufunga magoli. Hata hivyo, ingawa nafasi hizo za namba nane na tisa huchezwa na watu tofauti, lakini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), Hamad Abdallah ameweza kucheza nafasi hizo mbili peke yake katika kuhakikisha anatimiza majukumu yake ya kuliongoza shirika hilo la taifa. Mkurugenzi huyo amecheza nambari nane kwani Oktoba hii ametimiza miezi minane tangu alipoteuliwa na Rais Samia kuiongoza NHC Februari 23, mwaka huu akichukua nafasi ya Nehemia Mchechu, ambaye ameteuliwa kuwa Msajili wa Hazina. Si hivyo tu, bali Hamad pia amehitimisha ziara ya mikoani ambapo ametoa maagizo na maelekezo nane yenye lengo la kulisukuma mbele shirika h...