Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetua katika Jimbo la Uchaguzi Mtambwe, Zanzibar kwa kumteua kada wake, Hamad Khamis Hamad kuwania kiti cha uwakilishi.
Jimbo la Mtambwe linatarajiwa kufanya uchaguzi mdogo Oktoba 28 mwaka huu, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwakilishi wake, Habib Mohammed Ali, aliyefariki mwezi Machi mwaka 2023.
Taarifa ya uteuzi huo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imetangazwa Oktoba Mosi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema, kufuatia kikao chake maalum.
Hamad anatarajiwa kupambana na wagombea kutoka vyama vingine ikiwamo Dk Mohammed Ali Suleiman wa ACT Wazalendo, kilicho na ushindani mkubwa na CCM visiwani Zanzibar.
0 Maoni