Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MO Dewji aongoza matajiri vijana Afrika


Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

 Mfanyabiashara Mohammed Dewji maarufu MO Dewji, ametajwa kinara kwa utajiri miongoni wafanyabiashara vijana barani Afrika, akiwa na utajiri unaofikia Dola za Marekani bilioni 1.5, sawa na takriban shilingi trilioni 3.75.

Dewji pia anatajwa kuwa ndiye milionea kijana zaidi katika orodha hiyo ya matajiri kumi viana barani Afrika kufikia Oktoba 2023, akiwa na umri wa miaka 48. Anayemfuatia ana umri wa miaka 61 huku wa kumi akiwa na miaka 70.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Business Insider Africa, utajiri wa Dewji, ambaye pia anamiliki asilimia 49 ya hisa katika Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, unatajwa kutokana na biashara mbalimbali anazozifanya ndani na nje ya Tanzania.

Mfanyabiashara, Mohammed Dewji

Ripoti hiyo inamtaja MO ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Limited (MeLT Group), anatajwa kushika nafasi ya 13 katika orodha ya matajiri wote barani Afrika.

Mfanyabiashara maarufu hapa nchini Aliko Dangote(66) raia wa Nigeria, naye ametajwa katika orodha hiyo, akishika nafasi ya nane kutokana na biashara mbalimbali ikwamo saruji. 

Dangote anamiliki kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara. Katika orodha hiyo  anatajwa kumiliki ukwasi unaofikia Dola za Marekani bilioni 13.5 sawa na wastani wa shilingi trilioni 33.75.

Dewji anafuatiwa na Patrice Motsepe kutoka Afrika Kusini, mwenye umri wa miaka 61, anayetajwa kuwa tajiri kijana wa pili Afrika, akiwa na utajiri wa Dola za Marekani 3.2 sawa na takriban Sh. bilioni 8. Motsape ni mfanyabiashara wa madini na Mwenyekiti wa Kampuni ya African Rainbow Minerals ya Afrika Kusini.

Nafasi ya tatu ya matajiri vijana Afrika inashikiliwa na Nassef Sawiris wa Misri, ambaye ana umri wa miaka 62, akiwa na utajiri unaofikia Dola bilioni 7 sawa na shilingi trilioni 17.5, akitajwa kujishughulisha na biashara ya ujenzi na uwekezaji Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Kwa mujibu wa Business Insider Africa, Strive Masiyiwa (62) wa Zimbabwe, ndiye tajiri wa nne kijana Afrika na anamiliki utajiri wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.8 sawa na Sh. trilioni 45, akiwa na biashara ya kampuni ya simu, inayofanya kazi nchi kadhaa za Afrika.

Aziz Akhannouch wa Morocco ambaye pia ana umri wa miaka 62, ndiye tajiri wa tano kijana Afrika kwani anamiliki jumla ya Dola bilioni 1.5, sawa na takriban Sh trilioni 3.75 kutokana na bishara ya mafuta.

Anayeshika nafasi ya sita kwa utajiri akiwa kijana ni Yasseen Mansour(62), wa Misri kwa kumiliki Dola za Marekani bilioni 1.3 (Sh. trilioni 3.25) kutokana na biashara na uwekezaji mbalimbali.

Wa saba ni  raia wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu (63) aliye na ukwasi unaofikia dola za Marekani bilioni 6.9 sawa na shilingi trilioni 17.25 kutokana na biashara ya saruji na sukari.

Katika orodha hiyo Naguib Sawiris (69) wa Misri, anamiliki Dola za Marekani bilioni 3.3 kutokana na biashara ya kampuni ya mawasiliano billion.

Orodha hiyo inamtaja Mike Adenuga(70) akiwa na ukwasi unaofikia Dola bilioni 6.3(Sh.bilioni 15.75 kutokana na biashara ya mafuta na kampuni ya simu.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni