-Victoria, Nyasa, Tanganyika kucheka
Exuperius Kachenje, daimatzanews@gmail.com
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), limejipanga kupunguza na kuzuia athari za ajali majini, ikitangaza miradi mitatu mikubwa, ikiwamo wa ujenzi wa boti tano za uokoaji katika Ziwa Victoria,Tanganyika na Ziwa Nyasa.
Kuhusu hatua ya TASAC kupunguza na kuzuia athari za ajali majini, Mlali amesema: "Shirika linaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu mikuu ikiwamo ujenzi wa boti tano za uokoaji. Mbili kati ya hizo zitafanya kazi Ziwa Victoria, nyingine mbili Ziwa Tanganyika na moja Ziwa Nyasa."
Hatua hiyo inaashiria watumiaji wa maziwa hayo nchini yenye sifa za kipekee Afrika na duniani, wakapata faraja katika uendeshaji shughuli zao za kila siku katika uvuvi na usafirishaji kwa kuwa na uhakika wa kupata msaa inapotokea ajali.
Aliutaja mradi wa pili kuwa ni wa kimataifa wa mawasiliano na uchukuzi katika Ziwa Victoria (MLVMCT), unaotarajiwa kukamilika Desemba, 2024, huku wa tatu ukiwa wa uendelezaji na uimarishaji wa miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
![]() |
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari wakifuatilia mkutano na TASAC uliofanyika jijini Dar es Salaam Oktoba 5,2023. |
Katika mkutano huo ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina, Kaimu Mkurugenzi huyo wa TASAC aliutangazia umma fursa zilizopo kuwa ni pamoja na kuanzisha usajili wa meli kwa masharti rafiki (open registry), uanzishwaji wa maeneo ya ukarabati na ujenzi wa meli katika Ukanda wa Pwani.
Nyingine ni uanzishwaji wa maegesho ya boti ndogo katika Ukanda wa Pwani, uanzishwaji wa viwanda vya utengenezaji malighafi za ujenzi wa boti za plastiki, ujenzi wa bandari rasmi za uvuvi na kukidhi mahitaji ya soko la Comoro.
Hata hivyo, Mlali amesema kuwa TASAC inakabiliana na changamoto kuu mbili alizozitaja kuwa ni mabadiliko ya haraka ya teknolojia katika sekta na mahitaji makubwa ya mifumo ya TEHAMA;
"Uhaba wa wataalamu wa ndani katika baadhi ya taaluma hasa wakaguzi wa usalama wa vyombo vya usafiri majini,hii ni moja ya changamoto kubwa ya TASAF," amesema.
Akieleza namna TASAC inavyokabiliana na changamoto hizo, Kaimu Mkurugenzi huyo amesema wamejidhatiti kwa kukamilisha uundaji wa mifumo ya TEHAMA itakayowezesha kuwasiliana na mfumo mkuu wa pamoja wa wadau wa usafari majini.
Mlali anaongeza: "Pia tunakabiliana kwa kushirikiana na vyuo na taasisi mbalimbali vinavyotoa mafunzo ya ubaharia kikiwemo Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), katika kuongeza uwezo na wigo wa kutoa mafunzo na kuzalisha wataalam wanaohitajika."
Anataja utoaji elimu endelevu kwa umma ili waweze kuifahamu sekta ya usafiri majini na kuwavutia kutoa mchango wao katika maendeleo ya sekta kuwa ni namna nyingine ya kukabili changamoto hizo.
Mlali amesema katika kukuza ujuzi na kuchochea maendeleo ya watu kuna umuhimu wadau wote wa sekta ya usafiri kwa njia ya maji kushirikiana ili kuliwezesha taifa kufaidika zaidi na bahari, maziwa, mito, hata mabwawa yaliyopo nchini.
0 Maoni