-Ubalozi wa Sweden, SCF nguvu moja
Exuperius
Kachenje, daimatznews@gmail.com
Asilimia
6.5 ya wagonjwa wote wa saratani nchini wametajwa kuwa ni wanaume, ikielezwa
kwamba idadi hiyo ni mara kumi zaidi inayoonekana nchi nyingi duniani.
Balozi
wa Sweden nchini, Charlotta Ozaki amebainisha hayo katika mkutano wake na
wanahabari katika ofisi za ubalozi huo Dar es Salaam Oktoba 13, 2023, ambapo
pamoja na maadhimisho ya miaka 60 ya ubalozi huo nchini, alizungumzia ushiriki
wao katika kampeni ya kupambana na saratani ya matiti nchini.
“Tunataka
kuongeza ufahamu kuhusu saratani ya matiti kwa wanaume hata wavulana na
kuwasaidia wanawake. Tunataka watu wajifunze, saratani ya matiti sio ugonjwa wa
wanawake tu, wanaume pia huathiriwa,” alibainisha Ozaki.
Balozi huyo alisema: “ Ni muhimu kwetu kuwepo
hapa, mwezi huu Oktoba ni mwezi wa saratani ya matiti. Tupo hapa ili
kusisistiza umuhimu wa kuongeza uelewa kuhusu saratani ya matiti na aathari
zake kwa jamii ya Watanzania.”
Kwa
mujibu wa Balozi Ozaki mwezi huo wa Oktoba ni muhimu kwao kwani kwa kushirikiana na taasisi ya Shujaa
Cancer Foundation(SCF), Wizara tya Afya kampuni ya kiswidi ya ELEKTA, Taasisi
ya Saratani Ocean Road(ORCI) na Shirika la Afya Duniani, wameandaa matembezi ya
kilometa sita ili kukusanya fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya saratani ya
matiti, yatakayofanyika oktoba 21 viwanja vya ORCI.
Amesema
saratani ya matiti ndiyo chanzo kikuu cha vifo vinavyohusiana na saratani kwa
wanawake duniani na kwamba wakati mwezi huo wa saratani ya matiti unapoadhimishwa
makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwapo
kwa wagonjwa wapya takriban milioni mbili na laki moja kwa mwaka.
“Zaidi ya vifo 600,000 vinaripotiwa kila
mwaka, huku asilimia 80 ya wagonjwa wa saratani ya matiti nchini Tanzania wakigundulika
wakati tayari wamefikia hatua ya tatu au nne, hali inayochangiwa na kukosekana
kwa programu za uchunguzi, utambuzi na matibabu duni kama vile chemotherapy,
upasuaji na tiba ya mionzi,” amesema.
Balozi
huyo ambaye pia ni shujaa wa saratani ya matiti, amesema pia kwamba nchini
Tanzania, saratani ya matiti imeripotiwa kwa kiasi kidogo katika miongo miwili
iliyopita, huku kukiwa pia na tafiti chache.
Balozi
huyo amesema iwapo hakutakuwa juhudi za dhati, ongezeko la visa vipya vya saratani
Tanzania linakadiriwa kufikia asilimia 82 ifikapo mwaka 2030.
Akizungumza
matembezi hayo ya Oktoba 21, Mkurugenzi
Mtendaji wa SCF, Gloria Kida amesema yanalenga kukuza uelewa kuhusu umuhimu wa
kupima saratani ya matiti na kujipima, pamoja na kusaidia walioathirika, umuhimu
wa utafiti, kuzuia, matibabu na kupona.
Kida
amesema, pamoja na maadamano hayo, wameandaa fulana maalum, zitakazouzwa katika
vituo vitakavyokuwapo Dar Free Market na Shoppers Plaza akitaja mawasiliano ya
namba za simu 0745 538079 kuwa yatasaidia anayehitaji kupata fulana hizo na
fedha zitakazopatikana zitatumika kununulia vifaa vya mazoezi kwa wagonjwa wa
saratani.
Amesema
watajifunza pia kuhusu teknolojia ya kisasa zaidi katika uchaguzi wa saratani
nchini iliyofadhiliwa na kampuni ya ELEKTA ya Sweden.
Amesema
ni muhimu kila mmoja akaonyesha mshikamano na kusaidia wagonjwa na waathirika
wa saratani ya matiti bila kuwasahau wahudumu wa saratani.
0 Maoni