Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Mchakato wa kumtangaza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kuwa Mtakatifu unaoratibiwa na Katisa Katoliki nchini, umepiga hatua moja mbele kutoka ya awali, ukitajwa kuingia hatua muhimu zaidi.
![]() |
| Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere |
Taarifa kutoka ndani ya kanisa hilo zinaeleza kuwa mchakato huo sasa umefikia hatua ya mashahidi kuhojiwa rasmi kuhusu maisha ya imani na maadili ya Kikristo ya Mtumishi wa Mungu huyo, Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania.
Taarifa zinapasha kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Henry Mchamungu, ndiye anayesimamia kikao cha kikanisa kuhusu mchakato huo akinukuliwa kueleza hatua iliyofikiwa sasa ya muhimu sana.
"Hii ni kwa sababu ushahidi wa mashahidi utathibitisha sifa za utakatifu na uadilifu wa Nyerere. Kila shahidi anahojiwa kwa maswali mengi ili kujenga ushahidi wa kuwasilishwa Vatican," amesema.
![]() |
| Askofu Msaidizi Henry Mchamungu |
Hatua za kumtangaza Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki Oktoba mwaka 1999 kuwa Mtakatifu baada ya kuiongoza Tanzania kwa miaka 25 kabla ya kustaafu mwaka 1985, mchakato wake ulianza mwaka 2005.
Hatua hiyo ilifuatia Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani wa wakati huo, Papa Benedict XVI kumtangaza Nyerere kuwa Mtumishi wa Mungu (Servant of God).
Hatua hiyo ya kutangwazwa Mtumishi wa Mungu ni ya kwanza kuelekea utakatifu.
Mchakato huo wa kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu, awali ulisimamiwa na Jimbo Katoliki la Musoma kabla ya kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam mwaka 2014.
Hatua hiyo inatajwa kuhamia Jimbo Kuu la Dar es Salaam, baada ya kusuasua kwa miaka kadhaa, ambapo ulifufuliwa tena mwaka 2023.
Nyerere, aliiongoza Tanzania akiwa Rais wa Tanzania tangu Tanzania Bara ilipopata uhuru mwaka 1961 na baadae kuungana na Zanzibar mwaka 1964, hadi alipon'g'atuka madarakani mwaka 1985.
Kiongozi huyo alifariki dunia Oktoba 4 Oktoba 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London, Uingereza takribani miaka 27 iliyopita.


Chapisha Maoni