Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi
Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com
Tanzania imepiga hatua isiyosahaulika katika historia ya maendeleo yake, baada ya kikosi cha wawekezaji wa ngazi ya juu kutoka Ufalme wa Oman, kufanya ziara nchini na kukutana na uongozi wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), wakifungua fursa kubwa za mabadiliko makubwa katika sekta ya nyumba na maendeleo ya miji nchini.
![]() |
Ujumbe wa Wawekezaji kutoka Oman(kulia) ukiwa katika mkutano na uongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), (kushoto), makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam Mei 20,2024. |
Ujumbe huo uliongozwa na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Saud Al Shidha, ulikuwa na malengo kadhaa ya kukuza ushirikiano wa kiuchumi ikiwamo kuanzisha mabadiliko ya kimkakati, yatakayochochea ukuaji wa sekta ya makazi kwa njia ya ubia wa kimataifa.
Katika kikao cha kihistoria kilichofanyika Makao Makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) – Kambarage House, ujumbe wa Oman ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah, pamoja na viongozi waandamizi wa shirika hilo.
Mazungumzo yao yalilenga kuibua fursa za uwekezaji katika miradi ya nyumba za gharama nafuu, miundombinu ya kisasa ya miji, na kuanzisha ushirikiano thabiti baina ya sekta binafsi na ya umma (PPP).
Katika mkutano huo, Sera ya Ubia ya NHC ya mwaka 2022 imekuwa nguzo muhimu iliyovutia wawekezaji kama Oman kuwekeza katika miradi yenye tija zaidi kwa Watanzania. Miradi hiyo inalenga sio tu kujenga makazi ya bei nafuu, bali pia kuongeza ajira kwa Watanzania katika nyanja mbalimbali za ujenzi, usimamizi wa miradi na usambazaji wa vifaa vya ujenzi.
Balozi Saud Al Shidha amesisitiza kuwa ushirikiano huo unafungamanisha historia ndefu ya uhusiano wa kifamilia na kiutamaduni baina ya Oman na Tanzania, akiongeza kuwa zaidi ya Waomani 10,000 wenye asili ya Kitanzania wanaishi Oman. “Uhusiano wetu si wa kibiashara tu, bali ni wa damu na historia. Tunalenga kuendeleza maendeleo endelevu kupitia miradi ya pamoja,” amesema Balozi Shidha.
Kwa upande wake, Hamad Abdallah amesema: “Huu si uwekezaji wa kawaida – ni mwanzo wa mapinduzi ya kimkakati katika sekta ya makazi nchini Tanzania. Watanzania wataona mabadiliko makubwa ndani ya muda mfupi.
Kwa upande wake, Nikolay Anuashvili, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Uwekezaji ya Oman, amesema: “Tunajenga daraja la matumaini na ushirikiano wa kweli kati ya mataifa yetu. Lengo letu ni kuleta makazi bora, miji bora, na maisha bora kwa Watanzania.”
![]() |
NHC imesisitiza kuwa ushirikiano huo ni fursa kwa Watanzania wote, hasa wajasiriamali wa sekta ya ujenzi, wasambazaji wa vifaa, wafanyabiashara wa ndani na wananchi wanaotafuta makazi bora na ya gharama nafuu.
NHC inawanahimiza wananchi wenye nia kujiandikisha kwenye tovuti rasmi ya NHC ili kushiriki kikamilifu katika mabadiliko haya makubwa.
Kuhusu mshikamano wa kitaifa na ushirikiano wa kimataifa, NHC imesema Tanzania inaelekea kwenye enzi mpya ya maendeleo ya makazi, ikichochewa na dira thabiti ya shirika hilo na wawekezaji wa Oman.
Limesema hio ni mwanzo wa mapinduzi ya kweli katika sekta ya makazi, na Watanzania wote watarajir mafanikio makubwa yanayokuja haraka.
Maoni
Chapisha Maoni