RAIS DK. SAMIA, MAASKOFU KATOLIKI WATETA IKULU

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amekutaka na kuzungumza na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), leo Agost 10-2026 na kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Taifa.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, imeeleza kuwa Rais Samia amekutana na ujumbe huo wa TEC, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Taarifa hiyo ya Ikulu imebainisha kwamba pamoja na kujadili nafasi ya viongozi wa dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano mazungumzo mazungumzo ya pande hizo yamegusa masuala mbalimbali ya kitaifa.

Ikulu imetaja mabo hayo kuwa ni pamoja na yale yanayoigusa jamii, ikiwemo siasa, imani, maendeleo na umuhimu wa kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia amewashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.

"Rais amesisitiza umuhimu wa kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha viongozi wa dini pamoja na makundi mbalimbali katika jamii katika masuala yanayohusu ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa," imesema taarifa ya Ikulu na kuongeza:

"...Viongozi hao wamejadili pia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano."

Taarifa ya Ikulu imefafanua kwamba Rais Samia amesema ushirikiano huo ni sehemu muhimu ya kujenga Taifa lenye amani na mshikamano, huku akitambua mchango wa viongozi wa dini katika masuala mbalimbali yanayogusa maisha ya wananchi.

Mazungumzo hayo pia yameweka msisitizo katika umuhimu wa Serikali na viongozi wa dini kuendelea kuwa na majadiliano ya mara kwa mara kuhusu masuala yenye maslahi mapana kwa Taifa. 





Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi