Moshi mweusi watokea Vatican, moshi mweupe wasubiriwa kwa hamu

 -Makardinali wajifungia kwa siku ya pili

Mwaandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Vatican City,

Siku ya kwanza ya uchaguzi wa Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki (Baba Mtakatifu),imepita bila kupatikana Papa, baada ya mosi mweusi kutokea kwenye dohani ya kanisa dogo la Sistine kwenye picha ya mjongeo chini, mjini Vatican kuashiria kwamba siku ya kwanza imekwisha, lakini Papa hajapatikana. 


Ukitokea moshi mweupe, ni ishara kwamba Papa amepatikana, hivyo waumini hushangilia..

Kwa siku ya pili leo kuanzia jana Mei 7,2025, makardinali 133 wa Kanisa Katoliki duniani jana Mei 7, 2025 walianza mchakato wa kupiga kura kumtafuta Papa mpya.

Papa huyo mpya atakuwa mrithi wa nafasi hiyo ya kuliongoza Kanisa Katoliki, baada ya kifo cha mtangulizi wake, Papa Francis kilichotokea mjini Vatican Aprili 21,2025.

Mkutano huo maarufu kwa jina la Conclave unafanyika katika Kanisa dogo la

Makardinali wakiingia kanisani kwa ibada 

Sistine Chapel, Vatican City, makao makuu ya kanisa hilo, ambapo makardinali hao kutoka nchi mbalimbali hujifungia wakisali  na kuendesha mchakato huo ili kumpata kiongozi wao.

Kardinali Protas Rugambwa, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Tabora, pia anashiriki mkutano huo wa kihistoria ndani ya Kanisa Katoliki kumchagua Papa.

Papa hutambulika pia kama Halifa wa Mtume Petro, anayeaminika na Kanisa Katoliki kuwa ndiye kiongozi wa kwanza wa kanisa hilo, aliyechaguliwa na Yesu Kristo, kuchunga kundi la wanafunzi wake.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi