Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi yatangaza majimbo mapya 8 ya uchaguzi

-Dar sasa majimbo 8, mapya ni  Chamazi na Kivule

-Wabunge kuongezeka

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, (INEC), imetangaza majimbo mapya nane ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu ujao wa madiwani, wabunge na Rais, huku ikibadili majina ya majimbo tisa.

Mwenyekiti wa INEC,Jaji wa Rufaa, Jacob's C Mo Mwambegele 

Katika mabadiliko hayo yaliyotangazwa leo na tume hiyo, mikoa ya Dar es Salaam na Geita imefadiika zaidi kwa kuongezewa majimbo mawili kila mmoja, ambapo Dar es Salaam majimbo mapya ni Chamazi na Kivule, huku Geita mapya yakiwa Katoro na Chato Kusini. 

Kufuatia mabadiliko hayo, Dar sasa itakuwa na majimbo nane kutoka sita ya awali ambayo ni Ilala, Kinononi, Mbagala, Temeke, Ubungo na Kibamba, Chamazi (jipya) na Kivule (jipya).

Geita pia itakuwa na majimbo nane ambayo ni Chato Kusini, Chato Kaskazini, Katoro, Butundwe, Busanda, Nyang’wale, Mbogwe na Bukombe.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa,Jacob's C Mo Mwambegele  kupitia taarifa yake kwa umma leoJumatatu, Mei 12,2025 ameeleza kuwa wamefanya mabadiliko hayo kwa kuzingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na masharti ya Kanuni za tume hiyo.

Mikoa mingine iliyonufaika na mabailiko hayo ni pamoja na Dodoma ikipata Jimbo la Uchaguzi jipya la Mtumba, kutoka kugawanywa Jimbo la Dodoma Mjini, Mkoa wa Mbeya umepata Jimbo Jipya la Uchaguzi Uyole baada ya Kugawanywa Jimbo ya MjMkoa wa Simiyu limeanzishwa Jimbo Jipya la Uchaguzi Bariadi Mjini, baada ya la awali Bariadi k24ugawanywa na Shinyanga wamepata Jimbo Jipya la Uchaguzi Itwangi, kugawanywa.

Hatua hiyo ya INEC sasa itafanya idadi ya wabunge pia kuongezeka hasa Tanzania Bara ambapo watafikia 222 kutoka 214.

"Napenda kuwatangazia kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka 2025 jumla ya majimbo ya uchaguzi 272 yatatumika kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano. Kati ya majimbo hayo, 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar. Orodha ya majimbo yote itachapishwa kwenye Gazeti la Serikali," amesema Jaji Jacobs C Mo Mwambegele na kuongeza:

"Napenda kutangaza rasmi kwamba, jumla ya kata 3,960 zitatumika kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kata hizo 3,960 ni ongezeko la kata mpya tano (05) za Ngereyani na Sinonik katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido na kata za Mupi, Bwawani Mjini na Shela katika Halmashauri ya Mji Rufiji ambazo zilianzishwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa."

 HABARI ZAIDI SOMA KIAMBATANISHO CHINI..;   

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA             

                                          TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA YA MHESHIMIWA JAJI WA RUFAA JACOBS C Mo MWAMBEGELE
MWENYEKITI WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA UMMA
KUHUSU KUGAWA AU KUBADILI MAJINA YA MAJIMBO YA UCHAGUZI KWA 
UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ndugu waandishi wa habari!

1.0 UTANGULIZI

Kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na kifungu cha 10(1)(d) cha Sheriaø ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 2 ya Mwaka 2024, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imepewa mamlaka na jukumu la kuchunguza, kupitia mipaka na kugawa majimbo ya uchaguzi katika Jamhuri ya Muungano.

Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 18(1) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, kupitia vyombo vya habari, Tume ilitoa tangazo kuutaarifu umma kuhusu kuanza kwa mchakato wa kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi kuanzia tarehe 27 Februari hadi 26 Machi, 2025.

Tangazo hilo liliweka utaratibu na vigezo vitakavyozingatiwa na Tume wakati wa kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi. Kufuatia tangazo hilo Tume ilipokea jumla ya maombi thelathini na nne (34) ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi kumi (10) ya kubadili majina ya majimbo.

Ndugu waandishi wa habari!

Baada ya kupokea maombi na kwa kuzingatia kanuni ya 18 (5) ya Kanuni za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, Tume ilitembelea na kufanya vikao na wadau katika baadhi ya majimbo yaliyoomba kugawanywa pamoja na majimbo yote yaliyoomba kubadilishwa majina ili kujiridhisha na taarifa za maombi zilizowasilishwa Tume.

Leo tarehe 12 Meir 2025 tumewaita ili tuwatangazie majimbo mapya yaliyogawanywa, majimbo yaliyobadilishwa majina, idadi ya majimbo yote kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge na idadi ya kata zote kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani katika Uchaguzi wa Mwaka 2025.

2.0 MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI YALIYOANZISHWA Ndugu waandishi wa habari!

Pamoja na vigezo vya ugawaji wa majimbo vilivyoainishwa, Tume imezingatia zaidi vigezo vinne ambavyo imevipa uzito kwenye mchakato wa ugawaji wa majimbo. Vigezo hivyo ni:-  idadi ya watu, ambapo kwa majimbo ya mjini kigezo kilikuwa kuanzia watu

600,000 na kwa majimbo ya vijijini ilikuwa kuanzia watu 400,000;

b. uwezo wa ukumbi wa Bunge; kwamba kwa sasa ukumbi wa Bunge una uwezo wa kuchukua wabunge wapya wangapi;

c. idadi ya wabunge wanawake wa viti maalum; na

d. jimbo moja la uchaguzi kutokuwa katika wilaya au halmashauri

mbili. Kwa kuzingatia vigezo hivyo na masharti ya ibara ya 75(1), (2) na (4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa pamoja na kanuni ya 18(7) ya Kanuni za Turne Huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, baada ya kuchakata maombi husika, Tume imekubali na kuanzisha majimbo mapya nane (08) yafuatayo:

a. Mkoa wa Dar es Salaam yameanzishwa majimbo mawili kama ifuatavyo:-

 i. Jimbo la Uchaguzi la UKONGA limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la KIVULE; na ii. Jimbo la Uchaguzi la MBAGALA limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la CHAMAZI.

b. Mkoa wa Dodoma limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la DODOMA MJINI limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la Uchaguzi la MTUMBA.

c. Mkoa wa Mbeya limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la MBEYA MJINI limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la UYOLE

d. Mkoa wa Simiyu limeanzishwa jimbo jipya moja. Ambapo Jimbo la Uchaguzi la BARIADI limegawanywa na kuanzishwa jimbo jipya la uchaguzi la BARIADI MJINI.

e. Mkoa wa Geita yameanzishwa majimbo mawili kama ifuatavyo:-

i. Jimbo la Uchaguzi la BUSANDA limewaganywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la KATORO; na ii. Jimbo la Uchaguzi la CHATO limegawanywa na kuanzishwa Jimbo  jipya la Uchaguzi la CHATO

KUSINI

f. Mkoa wa Shinyanga limeanzishwa jimbo jipya moja, ambapo Jimbo la Uchaguzi la SOLWA limegawanywa na kuanzishwa Jimbo jipya la Uchaguzi la ITWANGI.

3.0 MAJIMBO YA UCHAGUZI YALIYOBADILISHWA MAJINA

Ndugu waandishi wa habari!

Tume imebadili majina ya majimbo ya uchaguzi kumi na mbili (12) kama ifuatavyo:   Mkoa wa Geita, Halmashauri ya Wilaya ya Chato: Baada ya kugawanywa Jimbo la CHATO na kuanzisha Jimbo jipya la uchaguzi la CHATO KUSINI. Jimbo la sasa la CHATO limebadilishwa jina, litaitwa Jimbo la Uchaguzi la CHATO KASKAZINI

b. Mkoa wa Kagera, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi: Jimbo la Uchaguzi la NKENGE limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la MISSENYI.

c. Mkoa wa Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika: Jimbo la Uchaguzi la MPANDA VIJIJINI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la TANGANYIKA.

d. Mkoa wa Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko: Jimbo la Uchaguzi la BUYUNGU limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la KAKONKO.

e. Mkoa wa Simiyu, Wilaya ya Bariadi: Baada Jimbo la BARIADI kugawanywa na kuanzisha Jimbo jipya la uchaguzi la BARIADI MJINI.

Jimbo la sasa la BARIADI limebadilishwa jina, litaitwa Jimbo la Uchaguzi la BARIADI VIJIJINI.

f. Mkoa wa Singida, majimbo matano yamebadilishwa majina kama  ifuatavyo:is Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni: 

Jimbo la Uchaguzi la MANYONI MASHARIKI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la MANYONI iie Halmashauri ya Wilaya ya Singida: 

Jimbo la Uchaguzi la SINGIDA KASIKAZINI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la ILONGERO.  

iii. Halmashauri ya Wilaya ya Itigi: Jimbo la Uchaguzi la MANYONI MAGHARIBI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la ITIGI 

iv. Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi: Jimbo la Uchaguzi la SINGIDA MASHARIKI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la IKUNGI MASHARIKI

v. Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi: Jimbo la Uchaguzi la SINGIDA MAGHARIBI limebadilishwa jina, sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la IKUNGI MAGHARIBI

g. Mkoa wa Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Uyui: Jimbo la Uchaguzi

la Tabora Kaskazini limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la

UYUI; na

h. Mkoa wa Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Vijijini: Jimbo la Uchaguzi la HANDENI VIJIJINI limebadilishwa jina sasa litaitwa Jimbo la Uchaguzi la HANDEN1û

4.0 IDADI YA MAJIMBO YA UCHAGUZI 

Ndugu waandishi wa habari!

Kutokana na kuongezeka kwa majimbo mapya ya uchaguzi nane (08) kama nilivyoeleza awali, napenda kuwatangazia kuwa katika Uchaguzi wa Mwaka 2025 jumla ya majimbo ya uchaguzi 272 yatatumika kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge, katika Jamhuri ya Muungano. Kati ya majimbo hayo, 222 yapo Tanzania Bara na majimbo 50 yapo Tanzania Zanzibar. Orodha ya majimbo yote itachapishwa kwenye Gazeti la Serikali.

5.0   KATA ZA UCHAGUZI

     Ndugu waandishi wa habari!

Kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 5(4) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024, napenda kutangaza rasmi kwamba, jumla ya kata 3,960 zitatumika kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani kwa Tanzania Bara katika Uchaguzi Wfkuu wa Mwaka 2025.

Kata hizo 3,960 ni ongezeko la kata mpya tano (05) za Ngereyani na Sinonik katika Halmashauri ya Wilaya ya Longido na kata za Mupi, Bwawani Mjini na Shela katika Halmashauri ya Mji Rufiji ambazo zilianzishwa na Waziri mwenye dhamana ya

Serikali za Mitaa.

Orodha ya kata zote za Tanzania Bara itachapishwa kwenye Gazeü la Serikali.


6.0 HITIMISHO

Ndugu waandishi wa habari!

Napenda kuturnia fursa hii kuwataarifu wananchi kuzingatia mabadiliko haya ya maeneo ya uchaguzi ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya kushiriki kugombea na kupiga kura siku ya kupiga kura.

Ndugu waandishi wa habari!!

Mwisho, napenda kutoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika awamu ya pili kwa mikoa kumi na sita (16) iliyobakia, kuhakiki taarffa zao katika Daftari la Awali la Wapiga Kura linalowekwa wazi katika kila kituo na kujiandaa vyema kwa ajili ya Uchaguzi

Mkuu wa Mwaka 2025.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

 


Jaji (Rufaa) Jacobs C. M. Mwambegele 

MWENYEKITI TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI 12 Mei, 2025 



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi

Moshi mweusi watokea Vatican, moshi mweupe wasubiriwa kwa hamu