WAZIRI WA NISHATI, SHELL, EQUINOR WAJADILI MRADI WA SH.40BIL CNG LINDI

-Lengo kuhakikisha unakekelezwa

Mwandishi Wetu
Waziri wa Nishati, Dk. Juma Zuberi Homera, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na kampuni za kimataifa zinazohusika na Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG), unaotekelezwa mkoani Lindi.
Dk. Homera ametoa kauli hiyo leo Oktoba 22,2026, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji na Mwenyekiti wa Kampuni ya Shell, Menno Bax pamoja na Hilde Merete Nafstad Makamu wa Rais wa Kampuni ya Equinor Tanzania.

huku akiwahakikishia kwamba Serikali itaendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha mradi huo muhimu kwa maslahi na ustawi wa taifa wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni42, sawa na takriban Shilingi Trilioni 113.4, unaanza kutekelezwa.
 
"Serikali inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa kwa kuwa ni miongoni mwa miradi muhimu itakayochangia upatikanaji wa nishati ya kutosha nchini, sanjari na kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, lengo letu ni kuona mradi unatekelezwa," amesema Homera.
Amesema Serikali inatambua umuhimu wa mradi huo kwa maendeleo ya taifa ikiwemo kuwezesha ukuaji wa viwanda, ajira, pato ya taifa na huduma za kijamii kwa wananchi wanaoishi kuzunguka eneo la mradi. 
 
Mradi huo wa LNG unaotarajiwa kutekelezwa mkoani Lindi na kampuni za kimataifa za Shell, Equinor, unazihusisha pia kampuni za ExxonMobil, Pavilion Energy na MedcoEnergi, zikiutekeleza kushirikiana na Serikali, kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), huku uwekezaji wake  ukifikia Dola za Marekani bilioni 42.
Waziri Dk. Homera pia amewataka wabia wa mradi huo kuhakikisha wanawashirikisha wananchi kwenye utekelezaji mradi huo kwa hatua mbalimbali ili nao wanufaike kupitia miradi ya maendeleo ya kijamii inayotekelezwa kwenye maeneo yanayozunguka mradi.

Kwa upande wao viongozi wa Kampuni za Shell na Equinor wameeleza kwamba kampuni zao zitaendelea kushirikiana na Serikali katika hatua mbalimbali za maandalizi na utekelezaji wa mradi huo. 
Wamesema kwamba mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na kampuni zinazoshiriki katika uwekezaji huo.
Katika hatua nyingine, Dk. Homera amepongeza ujenzi wa Shule ya Msingi Likong'o iliyojengwa kwa ushirikiano wa Kampuni za Shell, Equinor na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Kijiji cha Likong'o mkoani Lindi, ambako mradi huo unatarajiwa kutekelezwa. 



Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi