Imeichukua takriban siku 1,273 ambazo ni miezi 42, sawa na miaka mitatu na miezi mitano, kabla ya klabu ya Simba ya Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaaam, kurejesha ladha na heshima ya Dabi ya Kariakoo, baada ya kumfunga mtani wake wa jadi, Yanga ya Mitaa ya Twiga na Jangwani kwa magoli 2-1, katika mchezo uliochezwa Oktoba 10,2026, Uwanja wa Uhuru, maarufu Shamba la Bibi.
![]() |
| Mshambuliaji Peter Shalulile |
Mechi hiyo ya Oktoba 10, 2026 ilikuwa ya tisa kuwakutanisha watani hao wa jadi, huku historia ikionyesha kuwa katika michezo minane ya Ligi Kuu ya NBC iliyozikutanisha timu hizo kwa misimu minne mfululizo,Simba haikuwahi kuifunga Yanga.
Mechi hiyo ilianza kwa Yanga kuifunga Simba goli la mapema dakika ya tano ya mchezo, lililowekwa kimiani na Mshambuliaji wa Kimataifa wa Namibia, Peter Shalulile aliyekamilisha kazi nzuri ya Maxi Nzingeli. Hadi dakika 45 za kwanza kuhitimishwa Simba ilikuwa na nyuma kwa bao 1-0.
Hata hivyo, kipindi hicho kilishuhudiwa kiunga mkabaji wa Yanga, raia wa Kenya, Duke Abuya kuumia, hali iliyomlfanya kocha wa timu hiyo, Mangoba Mng'iti kufanya mabadiliko ya lazima kwa kumtoa Abuya na kumuingiza Fred Ngoma hatua ambayo hata hivyo, iliipa Simba nafasi zaidi ya kutawala eneo la kati la mchezo huo.
Hali hiyo iliendelea kuipa nguvu Simba ambayo ilirejea kipindi cha pili ikionyesha ubora zaidi kwa kulisakama lango la Yanga kupitia washambuliaji wake wakiongozwa na Elly Mpangu. ambapo dakika ya 68 ya mchezo Neo Maema aliisawazishia Simba, huku dakika ya 72, Elly Mpanzu akiiandikia Simba goli la pili na la ushindi, lililorejesha hadhi ya Dabi.
![]() |
| Mshambuliaji Ellie Mpanzu |
Msimu wa 2024/2025 mzunguko wa kwanza wa ligi Yanga ilishinda 1-0 na msimu wa pili ilishinda 2-0.
Hata hivyo mechi mbili za Ligi Kuu simu wa 2025/2026 timu hizo zilitoka sare ya 0-0 na Simba huku pia zikitoa sare 2-2 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
Timu hizo zitakutana tena katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC, huku swali likiwa; Je simba ataendelea alichokianzisha msiku huu, au Yanga itamzuia? Jibu litapatikana siku hiyo inayosubiriwa kwa hamu.


Chapisha Maoni