Vatican City,
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo XIV anatarajiwa kulazwa Hospitali ya Roma leo Oktoba12,2026 kwa ajili ya kuondolewa uvimbe kwenye mapafu.
Katika upasuaji wataalam wameeleza kuwa utaamua iwapo uvimbe huo unaweza kutolewa na kama matibabu mengine zaidi yanahitajika.
Papa Leo ameweka hadharani kuhusu tatizo kubwa la kiafya linalomhusu, tangu alipochaguliwa kuwa Papa miezi 17 iliyopita.
Baba Mtakatifu amefichua kuhusu ugunduzi wa uvimbe huo mdogo wakati wa sala yake ya Jumapili adhuhuri na kutangaza kwamba anataka uondolewe.
Vatican imesema Papa Leo XIV alitarajiwa kulazwa katika Hospitali ya Gemelli leo Jumanne asubuhi, lakini hakuna taarifa zaidi kuhusu muda wa upasuaji wenyewe.
Upasuaji huo, ambao kwa kawaida hufanywa mtu akiwa amepigwa ganzi ya jumla (mwili mzima), iwapo Papa Leo atafanyiwa, utamhitaji kukaa hospitalini kwa wiki moja.
Tayari Vatican imefuta mikutano ya hadhara ya Papa siku ya Jumatatu hadi Oktoba 20.
"Haya ni mambo yanayoweza kutibiwa vizuri sana," amesema Dk. Lorenzo Spaggiari, Mkurugenzi wa Upasuaji wa kifua katika Taasisi ya Ulaya ya Matibabu ya Saratani (EIO), ambaye hata hivyo hahusiki na matibabu ya Papa, lakini anayeifahamu timu ya madaktari ya Hospitali ya Gemelli.
Teknolojia ya roboti kutumika?
Spaggiari amesema anatarajia timu ya madaktari wa Gemelli kufanya uchunguzi wa biopsy ili kubaini kama Leo ana saratani ya mapafu, ikifuatiwa na kuondolewa kwa sehemu ya mapafu iliyo na uvimbe.
Amesema uchunguzi wote unaweza kufanywa kwa kutumia mbinu za roboti, na unaweza kufanywa mfululizo, huku mgonjwa akiwa amepigwa sindano ya ganzi na timu tofauti za wataalamu.
Chapisha Maoni