Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kunogesha ufunguzi wa Maadhimisho ya Nanenane kwa Kanda ya Kati utakayofanyika Agosti Mosi hadi 8, 2026, yaliyoandaliwa kwa pamoja kati ya Mkoa wa Dodoma na Singida, ambapo atakuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameeleza hayo leo mjini huo akieleza kuwa maandalizi ya Maadhimisho hayo yamefikia hatua nzuri akibainisha kuwa waoneshaji zaidi ya 800 na wajasiriamali 180 wamethibitisha kushiriki.
Mbele ya wanahabari, leo Julai 20, 2026, Senyamule amesema maonesho hayo yatafanyika Agosti 1 hadi 8 jijini Dodoma yakihusisha washiriki kutoka ndani na kimataifa lengo likiwa kuonesha teknolojia na fursa za kuongeza tija katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi.
Kwa mujibu wa Senyamule, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo Agosti 8, 2026.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma amesema Dodoma ipo salama akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi bila hofu na kuhudhuria maadhinisho hayo.

Chapisha Maoni