ASHA DACHI AMRITHI RIOBA TBC

 Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Asha Dachi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Asha Dachi Mkurugenzi Mkuu TBC

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari amekariri taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk.Moses Kusiluka ikieleza kwamba kabla ya uteuzi huo, Aisha Dachi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

 Asha Dachi anachukua nafasi iliyoachwa na Ayoub Rioba aliyemaliza muda wake.


Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi