RAIS AZINDUA UJENZI SGR KIGOMA-TABORA

Asema ni sehemu ya kutimiza ahadi, ataja mambo matatu muhimu
Mwandishi Wetu
Rais Samia Suluhu Hassan amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika bandari, viwanja vya ndege reli na barabara maeneo mbalimbali nchini unaojenga mfumo jumuishi wa uchukuzi na kuunganisha maeneo ya uzalishaji na masoko ya ndani na nje ya Tanzania akieleza kwamba ili kupata matokeo tarajiwa kuna mambo matatu yanayohitajika.

Akizungumz wakati akizindua ujenzi wa meli nne za mizigo, na kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma, pamoja na kukagua ujenzi wa gati jipya la abiria na uboreshaji wa gati la mizigo katika Bandari ya Kigoma, Rais Samia amesema hatua hiyo ni sehemu ya kutimiza ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Ameyataja mambo hayo akisema; "Ili tupate matokeo tunayotarajia kutoka kwenye miradi tunayotekeleza nchini, ninasisitiza mambo matatu;Tuendelee kudumisha amani, utulivu na umoja kwani ndiyo msingi wa maendeleo; Wananchi wajiandae kuchangamkia fursa zote zitokanazo na miradi hiyo; Wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama vilinde miradi yote kwani hujuma yoyote ni hasara kwa wananchi wote."

Amesema aliahidi tutaifufua Kigoma na kuirejeshea hadhi yake, ikiwa ni sehemu ya kutimiza ahadi hiyo, hatua ambayo inaimarisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara na uwekezaji, inapunguza gharama za usafiri na usafirishaji na kuzalisha ajira kwa wananchi. 


Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi