MIAKA 30 YA TRA; RAIS SAMIA ATAKA UWAJIBIKAJI KATIKA KODI

-Ataka TRA ikusanye kwa haki, Serikali itumie kwa uadilifu

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema uzalendo katika kodi lazima uwe wa pande zote, bila upande wowote kuachwa nyuma ikiwamo Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuikusanya kwa haki na Serikali kuitumia kodi hiyo kwa uadilifu.

Rais ametoa kauli hiyo,Julai Mosi, 2026 alipokuwa akizungumza katika hafla ya Maadhimisho ya Miaka 30 ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaliyokwenda sanjari na tukio la kihistoria la utoaji wa Tuzo za Rais kwa Walipakodi.

"Uzalendo katika kodi lazima uwe wa pande zote, mwekezaji alipe kodi kwa uaminifu, Mamlaka ya Mapato ikusanye kwa haki na Serikali itumie kwa uadilifu," amesema Rais Samia.

Amebainisha kuwa kodi zinazokusanywa na mapato mengine, ndizo zitakazoiwezesha Serikali kuendelea kuendesha baadhi ya huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Tuzo Mshindi wa
Jumla kutoka GEITA GOLD MINE ambaye ni Mlipakodi wa hiari zaidi wa kampuni na
mwenye kiasi kikubwa cha mchango wa mapato katika
mwaka wa fedha 2024/2025.


"Nathubutu kusema kuwa, kulipa kodi ni wajibu wa kila mmoja wetu katika kujenga Taifa linalojitegemea. Kulipakodi ni uzalendo na ushujaa kwa maendeleo na kujitegemea kwa Taifa letu," amesema.

Katika hafla hiyo, zilitolewa ni Tuzo ya Mlipakodi bora kwa walipakodi waliokidhi vigezo ili kuleta hamasa ya ulipaji kodi nchini na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.

Hafla hiyo pia ilishuhudia TRA ikiadhimisha miaka 30 tangu ilipoanzishwa Julai 1 1996, ambapo inasherehekea pia uhusiano mzuri iliyojenga kati yake na walipakodi kwa miongo mitatu na kuchangia maendeleo ya kila sekta katika nchi yetu. 

TRA imesema katika miaka yake 30,kulipa kodi ni uzalendi na ushujaa kwa maendeleo na kujitegemea kwa Taifa.



Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi