Mwandishi Wetu
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limewataka Watanzania kutumia fursa ya Maonyesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026) kwa kutembelea banda la shirika hilo ili kupata elimu, ushauri wa kitaalamu na taarifa sahihi kuhusu huduma, miradi ya makazi, biashara na uwekezaji inayotekelezwa na NHC.
Akizungumza katika maonyesho hayo, Kaimu Meneja wa Habari na Uhusiano wa NHC, Yahya Charahani, amesema NHC ni taasisi ya kimkakati yenye mtaji unaofikia Shilingi trilioni 6.2, ambayo kwa sasa inatekeleza miradi 14 ya kimkakati katika mikoa 12 nchini.
Amesema miradi inayotekelezwa inayolenga kuongeza upatikanaji wa makazi bora kwa wananchi, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuimarisha maendeleo ya miji.
"Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu ili kupata taarifa sahihi kuhusu huduma zetu, kujifunza taratibu za kununua na kupanga nyumba za shirika, lakini pia kufahamu fursa mbalimbali za uwekezaji ndani ya NHC. Wataalamu wetu wapo tayari kuwahudumia na kujibu maswali yote," amesema Charahani.
Naye Meneja wa Mauzo na Masoko wa NHC, Deogratius Batakanwa, amesema kwenye banda la NHC wananchi watapata fursa ya kufahamu miradi mikubwa iiliyo sokoni kwa sasa ukiwemo Kawe 711 Mixed-Use Development, Kijichi Residence, Samia Housing Scheme katika maeneo ya Medeli, Iyumbu na Njedengwa.
Naye Meneja wa Mauzo na Masoko wa NHC, Deogratius Batakanwa, amesema kwenye banda la NHC wananchi watapata fursa ya kufahamu miradi mikubwa iiliyo sokoni kwa sasa ukiwemo Kawe 711 Mixed-Use Development, Kijichi Residence, Samia Housing Scheme katika maeneo ya Medeli, Iyumbu na Njedengwa.
Nyingine ni Uluguru Plaza, Mkwakwani Plaza, Songea Mixed-Use Development, Tabora Commercial Complex, pamoja na miradi mingine ya makazi na biashara inayotekelezwa na NHC nchini.
Kwa mujibu wa Batakanwa, miongoni mwa miradi mikubwa inayotekelezwa na NHC ni Mradi wa Samia Housing Scheme, unaotekelezwa kwa awamu kwa gharama ya Shilingi bilioni 466.
"Sabasaba ni fursa ya kipekee kwa wananchi kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa NHC na kujionea fursa za makazi na uwekezaji zinazoweza kubadili maisha yao," amesema Batakanwa.



Chapisha Maoni