GAWIO KWA SERIKALI; NHC LACHANUA LIKIWEKA HISTORIA MBILI MPYA

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuchanua likiandika historia mbili mpya moja ikiwa  kutoa gawio la Shilingi Bilioni 10 kwa Serikali kwa mara ya kwanza, pili ni kuingia kwa mara ya kwanza katika kundi la taasisi za umma zilizotoa gawio la zaidi ya Shilingi Bilioni 10 kwa Serikali.

Hatua hiyo ya NHC inatajwa ni kudhihirika kwa kuwa na kiwango bora cha utendaji lakini pia sha kuimarika kwa utendaji wake na mchango wake katika uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa gawio kwa Serikali  na tuzo iliyoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Juni 30,2026, Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, amesema idadi ya taasisi zilizofikisha kiwango hicho imeongezeka kutoka taasisi sita za mwaka uliopita ambapo kwa mwaka huu zimefikia taasisi kumi kutokana na maboresho makubwa ya utendaji katika taasisi za umma.

Kwa mujibu wa Mchechu, mwaka uliopita taasisi hizo sita zilichangia jumla ya Shilingi Bilioni 267, ambapo kwa mwaka huu taasisi kumi zimechangia Shilingi Bilioni 481.

“Ongezeko hilo linaakisi mafanikio ya mageuzi na usimamizi madhubuti wa uwekezaji wa Serikali kwenye mashirika ya umma,” amesema Mchechu.

Akiizungumza kuhusu NHC, Mchechu amesema shirika hilo ni miongoni mwa taasisi mpya zilizoingia kwenye orodha hiyo mwaka huu, baada ya kutoa gawio la Shilingi Bilioni 10, tofauti na mwaka uliopita ambapo haikufikia kiwango hicho.

“Mafanikio haya yanaonesha namna NHC inavyoendelea kuimarisha utendaji wake wa kifedha, huku ikiendelea kutekeleza dhamira yake ya kujenga makazi bora, kuendeleza miradi ya kimkakati na kuongeza thamani kwa Serikali pamoja na wananchi,” amesema Mchechun a kuongeza;

“Hatua hii ni ushahidi kuwa uwekezaji wa Serikali kupitia NHC unaendelea kuzaa matunda, huku Shirika likiendelea kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta ya makazi na uchumi wa Taifa.”

 

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi