MBUNGE AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO DAR

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Mbunge wa Viti Maalum,Halima Idd Nassar amefariki dunia leo Jumapili Januari 18,2026 katika Hospitali ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alipokuwa akipatiwa matibabu. 

Marehemu Halima Idd Nassar

Taarifa ya Bunge imemnukuu Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu akitangaza kifo hicho na kutoa pole kwa familia ya marehemu, wabunge, ndugu, jamaa na marafiki.

Taarifa hiyo, imeeleza kuwa Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia, inaratibu mipango ya mazishi.

Katika hatua nyingine, Ofisi ya Bunge imetoa tangazo linaloeleza kuwa marehemu Halima Idd Nassar atazikwa leo  saa 10 jioni katika makaburi ya Kibada kwa Dole Kigamboni, jijini Dar es Salaam.

Marehemu Halima, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum akiwakilisha wafanyakazi, alikuwa mkazi wa Kigamboni, alizaliwa tarehe 12, Machi, mwaka 1980.


Taarifa rasmi ya Ofisi ya Bunge soma hapa chini;




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi