Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2025
Rais Samia afuta sherehe 9 Desemba
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
- Aagiza fedha zitumike kujenga miundombinu - Waziri Mkuu aagiza shughuli zirejee ndani ya siku 10 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameelekeza hakutakuwa na maadhimisho ya Sherehe za Uhuru Desemba 09 mwaka huu. Maelekezo hayo ya Rais Samia, yametolewa kwa niaba yake na Waziri Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba leo Novemba 24,2025 ambaye amesema Rais ameagiza fedha zilizotengwa ili kutumika katika sherehe hizo, zitumike kurekebisha miundombinu iliyoharibika kutokana vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 wakati wa Uchaguzi Mkuu. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya umma pamoja na mali zilizoathiriwa na vurugu iliyotokea Oktoba 29, 2025. Amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kuiona Tanzania inakuwa moja na kuendeleza umoja wa Watanzania Akizungumzia ziara yake Dk.Mwigulu amesema: "Nimepitia na kukagua uharibifu wa mali na miundombinu ya umma, huwezi kuamini kama tukio hili limetokea Tanzania." Amesema Wata...
Waziri Mkuu aagiza Kanisa la Ufufuo na Uzima
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
- Ataka liwekwe chini ya uangalizi kwa miezi sita Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima, lakini akataka liwekwe chini ya uangalizi kwa miezi sita. Waziri Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo, Novemba 24, 2025 Mbezi Dar es Salaam, alipokuwa akihutubia wananchi, baadha ya kukagua miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vurugu za Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025. " Kama kutatokea kiongozi amekosa, sasa atashughulikiwa yeye badala ya taasisi yake, maana imani ni kati ya mtu na Mungu wake sio askofu," amesema Mwigulu. Kanisa hilo ambalo kiongozi wake ni Askofu Josephat Gwajima, lilifungiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ikielezwa kwamba kiongozi wake alikiuka masharti ya usajili wake kwa mujibu wa sheria.
Rais Dk.Mwinyi, Dk.Nchimbi wakutana Z'bar
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mwandishi Wetu, Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyefika Ikulu ya Zanzibar kujitambulisha rasmi. Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi(Kulia), akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi. Rais Dk. Mwinyi amempongeza Dk. Nchimbi kwa kushika wadhifa huo na kumhakikishia ushirikiano wa kiwango cha juu katika utekelezaji wa masuala yote yanayohusu Muungano. Ameeleza kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika kuzipatia ufumbuzi changamoto za muda mrefu zilizokuwepo, na kusisitiza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuendelezwa kwa ajili ya kuimarisha Muungano kwa maslahi ya pande zote mbili. Kwa upande wake, Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa ushindi mkubwa wa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Zanzibar na kueleza matumaini yake ya kuiona Zanzibar ikiendelea kupiga hatua kubwa za maendel...
Miradi ya NHC Kijichi, Kawe 711, Kariakoo nguzo 3 za kipekee Dar
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
-Kitovu cha mapato NHC, maisha bora kwa wananchi -Mwanzo mpya wa makazi ya kisasa Dar -Usanifu unaoendana na Dira ya Taifa ya 2050 -Ubia sekta binafsi, ubunifu wa NHC vyafungua milango fursa mpya kiuchumi, kijamii Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuthibitisha nafasi yake kama mhimili wa mageuzi ya sekta ya makazi nchini. Kupitia miradi mikubwa ya kisasa maeneo mbalimbali nchini, NHC inaonyesha dhamira yake ya kuunga mkono ajenda ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora, salama na endelevu. Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah Katika Jiji la Dar es Salam, NHC kupitia miradi ya Samia Housing Scheme Kijichi, Kawe 711 na Mradi wa Ubia wa Kariakoo, imeleta sura mpya katika jiji hilo kupitia ujenzi wa nyumba za kisasa, matumizi ya teknolojia ya gharama nafuu na ushirikiano mkubwa na sekta binafsi, ili kuongeza kasi ya upatikana...
Zawadi za PIKU zafungua milango ya ujasiriamali kwa Watanzania
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Katika kudhihirisha kuwa teknolojia inabadilisha maisha ya Watanzania, Jukwaa la Kidijitali la PIKU limeendelea kutoa tabasamu kwa watumiaji wake baada ya kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi zikiwemo bodaboda, televisheni aina ya LG, simu mpya aina ya Samsung 06, manukato mbalimbali pamoja koponi za safari za Bolt. Washindi hao wamekabidhiwa zawadi zao hizo na viongozi wa Jukwaa hilo la Piku huku simulizi zao zikionesha namna bidhaa hizo zitakavyoweza kuwainua na kujikwamua kiuchumi. Jackson Ngonji ni mshindi wa Pikipiki maarufu bodaboda aina ya TVS HLX 125 anasema ushindi huo utakwenda kubadilisha maisha yake kwani atakitumia chombo hicho cha usafirishaji na kujipatia kipato cha uhakika kila siku na kujikwamua kiuchumi. Amesema bodaboda hiyo itamsaidia kujitegemea zaidi, kupunguza changamoto za kifedha na hata kuweka akiba kwa ajili ya familia yake kwani ataitumia kufanyia biashara ya usafirishaji wa abiria. Amesema anaishukuru Piku kwa kulet...
NHC yavunja rekodi miradi mikubwa ya makazi inayoibadili Tanzania
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
- Sh400 bilioni zawekezwa na NHC ikiongoza safari ya makazi bora -Ni kupitia Samia Housing Kijichi, Kariakoo PPP na Kawe 711 -Mabilioni yazalishwa kwenye miradi kabla muda kusudiwa - Wananchi waongeza kasi kununua nyumba -Miradi ya kimkakati yainua uchumi, yabadili mandhari ya mijini Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeendelea kujidhihirisha kama nguzo muhimu ya maendeleo ya makazi nchini, likiendelea kutekeleza miradi mikubwa na ya kimkakati inayolenga kuwawezesha Watanzania kumiliki nyumba za kisasa kwa gharama nafuu na katika mazingira salama. Mradi wa Samia Housing Scheme utakavyoonekana baada ya kukamilika. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, NHC limewekeza nguvu kubwa katika miradi ya ubunifu, teknolojia ya gharama nafuu na ushirikiano mpana na sekta binafsi, hatua ambayo imeongeza kasi ya upatikanaji wa makazi ya kudumu na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Hali halisi katika maeneo mbalimbali nchini inathibitisha mag...
Waziri Mkuu ateta na Katibu Mkuu TEC
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, leo Novemba 20, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima. Waziri Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba(Kulia), akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Padri Charles Kitima. Wawili hao wamekutana katika Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.
Wahariri wampongeza Machumu
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limempongeza Bakari Machumu kwa kuteuliwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu. Taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa jukwaa hilo, Deodatus Balile, imemtaja Machumu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, imeeleza kuwa mteule huyo ni mchapa kazi. Taarifa zaidi ya TEF hii hapa...;
Machumu ateuliwa Mkurugenzi Ikulu
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
- Tido Mhando mshauri, Nyalandu Balozi Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, amemteua Bakari Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Bakari Machumu Machumu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited(MCL), amechukua nafasi ya Sharifa Nyanga, ambaye atapangiwa kazi nyingine. Taarifa ya Ikulu ya leo Novemba 19,2025 iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk.Moses Kusiluka, imeeleza hayo na kuongeza kwamba, Rais Samia pia amemteua Tido Mhando kuwa mshauri wake Habari na Mawasiliano. Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza pia kwamba, Rais Dk Samia amemteua Lazaro Nyalandu kuwa Balozi. Taarifa kamili ya Ikulu, hii hapa chini;
Prof Shemdoe: Tuhakikishe wananchi wanapata huduma bora
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
OR-TAMISEMI Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Profesa Riziki Shemdoe amewataka watumishi na viongozi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa upendo, amani, mshikamano na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kuwaachia tabasamu kupitia huduma hizo zinazotekelezwa na Serikali. Akizungumza mara baada ya kupokelewa na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI katika makao makuu ya wizara hiyo Mtumba nje kidogo ya Jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuwaachia Watanzania tabasamu ifikapo mwaka 2030, na kusisitiza kuwa TAMISEMI ina jukumu la moja kwa moja katika kutimiza azma hiyo. Amesema watumishi wanapotekeleza majukumu yao katika ngazi ya mikoa, wilaya, halmashauri, kata, vijiji, mitaa na vitongoji wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, zinazoendana na mahitaji yao na kuwapa tabasamu linalotarajiwa linalopaswa kuanzia kwa watumishi wenyewe kupitia utendaji uliokamilika n...
Rais Dk.Samia aapisha mawaziri, awaonya
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua jana, hafla iliyofanyika leo Novemba 18, 2025, Ikulu Chamwino jijini Dodoma akiwataka kwenda kuwajibika na kuonya haoni tabu kubadili mawaziri. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Profesa Rikizi Shemdoe akiapa mbele ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 18, 2025. Akizungumza katika hafla hiyo, Rais Samia amesema mawaziri na manaibu wao hao wamekabidhiwa majukumu ya kuwatumikia wananchi, akiwataka kutanguliza utu na uwajibikaji miongoni mwao na mbele ya wananchi. ”Kazi ya kuanzia sasa ni kuendelea kuwajibika kwa Taifa, viongozi wazito punguzeni uzito ili kwenda sambamba na kasi ya utekelezaji kwa kuwa muda ni mchache,” amesema. Kwa mujibu wa Rais Samia, Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza imepanga kuanza kutekeleza miradi kwa kutumia fedha za ndani na mashirika ya maendeleo yawakute wameshaanza utekeleza...
Kesi ya Benki Yetu dhidi ya BoT, NMB leo tena
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
-Ni ya kudai warejeshewe benki yao -Wadai mabilioni ya shilingi Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Kesi ya madai namba 24650 ya mwaka 2025 inayowahusisha wanahisa wa Benki ya Biashara ya Yetu, dhidi ya Benki Kuu ya Tanzania, Benki ya NMB na Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kusikilizwa leo Makahama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Emmanuel Tutuba Wanahisa wa Benki ya Biashara Yetu ni Taasisi ya Vijana ya Yosefo, Cornelius Kasiya Kariwa na Altemius Ambros Milinga, ambao katika kesi hiyo wanaongozwa na Wakili Ibrahim Bendera, aliyeieleza Mahakama kwamba wateja wake ambao ni wanahisa zaidi ya 12,000 wanadai Benki Kuu imekiuka sheria kwa kuichukua Benki ya Yetu na kuwapa Benki ya NMB, bila ya kuwalipa wanahisa hao thamani ya hisa zao. Wakili Bendera amesema katika kesi hiyo, wanahisa hao pia wanadai warudishiwe benki hiyo pamoja na pesa zao zote ziizokuwa benki, kiasi cha Sh6.18 bilioni. Amesema Benki hiyo ilikuwa i...
Baraza la Mawaziri hili hapa
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
- Dk.Biteko, Jenister, Jafo,Bashe waachwa -Prof. Shemdoe, Makonda, Nanauka wang'ara Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com Imemchukua takriban dakika nane, Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza Baraza lake jipya la Mawaziri uteuzi alioufanya kwa mujibu wa Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku sura mpya za vijana zikichomoza na mawaziri waliokuwa maarufu katika baraza lililopita wakiwekwa kando. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan Baadhi ya sura mpya za vijana zilizoibuka na kung'ara ni Joel Nanauka aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Vijana, Prof. Riziki Shemdoe(Waziri wa TAMISEMI), Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni na Michezo na Wanu Hafidh Ameir (Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia) Baadhi ya walioachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko, Jenister Mhagama (Wazira wa Afya), Pindi Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hussein Bashe aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Stergomena Tax aliyekuwa W...