Machumu ateuliwa Mkurugenzi Ikulu
-Tido Mhando mshauri, Nyalandu Balozi
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, amemteua Bakari Machumu kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Machumu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), na aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited(MCL), amechukua nafasi ya Sharifa Nyanga, ambaye atapangiwa kazi nyingine. Bakari Machumu
Taarifa ya Ikulu ya leo Novemba 19,2025 iliyosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk.Moses Kusiluka, imeeleza hayo na kuongeza kwamba, Rais Samia pia amemteua Tido Mhando kuwa mshauri wake Habari na Mawasiliano.
Taarifa hiyo ya Ikulu imeeleza pia kwamba, Rais Dk Samia amemteua Lazaro Nyalandu kuwa Balozi.
Taarifa kamili ya Ikulu, hii hapa chini;

Maoni
Chapisha Maoni