Rais Dk.Mwinyi, Dk.Nchimbi wakutana Z'bar
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi, aliyefika Ikulu ya Zanzibar kujitambulisha rasmi.
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi(Kulia), akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi.
Rais Dk. Mwinyi amempongeza Dk. Nchimbi kwa kushika wadhifa huo na kumhakikishia ushirikiano wa kiwango cha juu katika utekelezaji wa masuala yote yanayohusu Muungano.
Ameeleza kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika kuzipatia ufumbuzi changamoto za muda mrefu zilizokuwepo, na kusisitiza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuendelezwa kwa ajili ya kuimarisha Muungano kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi amempongeza Rais Dk. Mwinyi kwa ushindi mkubwa wa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Zanzibar na kueleza matumaini yake ya kuiona Zanzibar ikiendelea kupiga hatua kubwa za maendeleo katika miaka mitano ijayo.
Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi(Kulia), akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati Makamu wa Rais alipomtembela Ikulu Zanzibar
Amesisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuendeleza Muungano kuwa imara zaidi.
Maoni
Chapisha Maoni