Waziri Mkuu aagiza Kanisa la Ufufuo na Uzima

-Ataka liwekwe chini ya uangalizi kwa miezi sita

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com 

Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, amemwagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kulifungulia Kanisa la Ufufuo na Uzima, lakini akataka liwekwe chini ya uangalizi kwa miezi sita.

Waziri Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo, Novemba 24, 2025 Mbezi Dar es Salaam, alipokuwa akihutubia wananchi, baadha ya kukagua miundombinu iliyoharibiwa wakati wa vurugu za Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

" Kama kutatokea kiongozi amekosa, sasa atashughulikiwa yeye badala ya taasisi yake, maana imani ni kati ya mtu na Mungu wake sio askofu," amesema Mwigulu.

Kanisa hilo ambalo kiongozi wake ni Askofu Josephat Gwajima, lilifungiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani, ikielezwa kwamba kiongozi wake alikiuka masharti ya usajili wake kwa mujibu wa sheria.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi