Kesi ya Benki Yetu dhidi ya BoT, NMB leo tena

 -Ni ya kudai warejeshewe benki yao

-Wadai mabilioni ya shilingi

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Kesi ya madai namba 24650 ya mwaka 2025 inayowahusisha wanahisa wa Benki ya Biashara ya Yetu, dhidi ya  Benki Kuu ya Tanzania, Benki ya NMB na Mwanasheria Mkuu wa Serikali itaendelea kusikilizwa leo Makahama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) Emmanuel Tutuba

Wanahisa wa Benki ya Biashara Yetu ni Taasisi ya Vijana ya Yosefo, Cornelius Kasiya Kariwa na Altemius Ambros Milinga, ambao katika kesi hiyo wanaongozwa na Wakili Ibrahim Bendera, aliyeieleza Mahakama kwamba wateja wake ambao ni wanahisa zaidi ya 12,000 wanadai Benki Kuu imekiuka sheria kwa kuichukua Benki ya Yetu na kuwapa Benki ya NMB, bila ya kuwalipa wanahisa hao thamani ya hisa zao.

Wakili Bendera amesema katika kesi hiyo, wanahisa hao pia wanadai warudishiwe benki hiyo pamoja na pesa zao zote ziizokuwa benki, kiasi cha Sh6.18 bilioni.

Amesema Benki hiyo ilikuwa inahudumia Watanzania wa Bara na visiwani zaidi ya 200,000 katika mikoa nane nchini.

Wanadai walipwe Sh 6.18 billioni pamoja na riba ya tangu benki yao ilipochukuliwa; walipwe na Benki Kuu na NMB fidia kwa madhara ya jumla Sh2 billioni, malipo ya Sh3 billioni kwa madhara waliopata wanahisa namalipo mengine kama Mahakama itakavyoona inafaa

Mapema wiki iliyopita Wakili wa wadai katika kesi hiyo ya madai aliiomba Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kusikiliza kesi hiyo upande mmoja dhidi ya  wadaiwa wawili kati ya watatu.

Wakili Bendera alitoa ombi hilo baada ya wadaiwa kushindwa kuwasilisha utetezi wao wa maandishi ndani ya muda unaotakiwa.

Mbele ya Jaji Mfawidhi Salma Maghimbi, Wakili Bendera aliieleza mahakama kwamba wadaiwa wote watatu walipelekewa wito wa mahakamani Oktoba 2, 2025, hivyo walikuwa na muda wa kutosha kuwasilisha utetezi wao, lakini ni mdaiwa mmoja tu ambaye ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliyewasilisha utetezi wake ndani ya muda.

Benki hiyo ilikuwa inahudumia Watanzania wa Bara na visiwani zaidi ya 200,000 katika mikoa nane nchini.

 

Madhara maalum tzs 6.18 billioni pamoja na riba ya Toka benki ichukuliwe;

Madhara ya jumla Tzs 2 billioni ilipwe na Banki Kuu na NMB

MALIPO ya 3 billioni  Kwa madhara waliopata wanahisa. Na MALIPO mengine kama Mahakama itakavyoona inafaa

 

Mdaiwa wa kwanza ambaye ni Benki Kuu ya Tanzania, yeye amewasilisha utetezi wake nje ya muda, wakati mdaiwa wa pili ambaye ni Benki ya NMB yeye hakuwasilisha kabisa utetezi wake.

Mbele ya mahakama hiyo kwa niaba ya Benki Kuu, Wakili wa Serikali Catherine Kiiza aliiomba Mahakama ikubali kupokea utetezi wa BoT ingawa umewasilishwa nje ya muda uliotakiwa.

Hata hivyo, Wakili huyo hakuelezea hoja au sababu za msingi za kuchelewa kwa utetezi wa BOT zaidi ya kumuomba Jaji aongeze muda.

Naye Wakili Mrano Mlekano  kwa niaba ya Benki ya NMB aliiomba Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kuwaongezea siku moja, ili aweze kuwasilisha utetezi wake kwa madai kwamba alishindwa kufanya hivyo kutokana na vurugu za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.

Alitaja sababu nyingine ni kuwepo kwa taarifa na nyaraka muhimu ambazo zilikua na zuio la kuonekana na watu wengine, hadi kupata ruhusa kutoka kwa Ofisa Fedha Mkuu wa NMB na Kitengo cha Uzingatiaji Kanuni (Compliance) cha Benki kuu.

 

Hata hivyo, Wakili Bendera alipinga hoja hizo na kueleza kuwa wadaiwa walikuwa na muda wa kutosha kuwasilisha utetezi wao na kumuomba Jaji Maghimbi aanze kusikiliza upande mmoja ambao umewasilisha utetezi wake ndani ya muda.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai, mara baada ya kupokea wito wa mahakama, mdaiwa anatakiwa kujibu utetezi wake ndani ya siku 21.

Sheria hiyo pia inasema, iwapo muda huo utapita, basi mdaiwa anaweza kuomba kuongezewa siku saba.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi