Baraza la Mawaziri hili hapa

 - Dk.Biteko, Jenister, Jafo,Bashe waachwa

-Prof. Shemdoe, Makonda, Nanauka wang'ara

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Imemchukua takriban dakika nane, Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza Baraza lake jipya la Mawaziri uteuzi alioufanya kwa mujibu wa Ibara ya 50 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku sura mpya za vijana zikichomoza na mawaziri waliokuwa maarufu katika baraza lililopita wakiwekwa kando.

Rais Dk. Samia Suluhu Hassan

Baadhi ya sura mpya za vijana zilizoibuka na kung'ara ni Joel Nanauka aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Vijana, Prof. Riziki Shemdoe(Waziri wa TAMISEMI), Paul Makonda aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni na Michezo na Wanu Hafidh Ameir (Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia) 

Baadhi ya walioachwa ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko, Jenister Mhagama (Wazira wa Afya), Pindi Chana aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Hussein Bashe aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Stergomena Tax aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambaye hata hivyo hakugombea ubunge.

Hata hivyo, mkongwe William Lukuvi, amerejea ulingoni baada ya kuteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, huku Prof. Palamagamba Kabudi akirejea katika nafasi ya uwaziri kwenye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Angela Kairuki akiwa Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Akizungumza na wanahabari, Ikulu ya Chamwino Dodoma, leo Jumatatu Novemba 17, 2027 Rais Samia amesema; " Juzi nilipozungumza na Bunge, nilisema sitachukua muda mrefu, nitaunda Baraza la Mawaziri."

"Ujio wangu hapa ni kuwataja wale watakaotusaidia kwenye kazi hizo za Mawaziri na Manibu Mawaziri. Lakini niseme kwa ujumla niseme tu, tumeona umuhimu wa vijana kuwa na wizara kamili ambayo itasimama nao.Wizara hii itakuwa chini ya Ofisi ya Rais," amesema Rais Samia.

𝐁𝐚𝐫𝐚𝐳𝐚 𝐥𝐚 𝐌𝐚𝐰𝐚𝐳𝐢𝐫𝐢 𝐥𝐢𝐥𝐢𝐥𝐨𝐭𝐚𝐧𝐠𝐚𝐳𝐰𝐚 𝐧𝐚 𝐑𝐚𝐢𝐬 𝐒𝐚𝐦𝐢𝐚 𝐒𝐮𝐥𝐮𝐡𝐮 𝐇𝐚𝐬𝐬𝐚𝐧 ni hili hapa chini;

I. Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

a)    Waziri: Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete

b)    Naibu Waziri: Mhe. Regina Ndege Qwaray

2.      Ofisi ya Rais — Mipango na Uwekezaji

a)                                                       Waziri: Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Pius Stephen Chaya

3.      Ofisi ya Rais - Maendeleo ya Vijana

a)                                                       Waziri: Mhe. Joel Arthur Nanauka

4.      Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira

a)                                                       Waziri: Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Dkt. Festo John Dugange

5.      Ofisi ya Waziri Mkuu — Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu

a)                                                       Waziri: Mhe. William Vangimembe Lukuvi

b)                                                      Ummy Hamisi Nderiananga

1

6.      Offsi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano

a)    Waziri: Mhe. Deus Clement Sangu

b)    Naibu Waziri: Mhe. Rahma Riadh Kisuo

7.      Ofisi ya Waziri Mkuu — Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

a)     Waziri: Mhe. Prof. Riziki Silas Shemdoe

b)    Naibu Waziri (Elimu): Mhe. Reuben Nhamanilo Kwagilwa

c)     Naibu Waziri (Afya): Dkt. Jafar Rajab Seif

8.      Wizara ya Fedha

a)     Waziri: Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar

b)    Naibu Waziri: Mhe. Laurent Deogratius Luswetula

c)     Naibu Waziri: Mhe. Mshamu Ali Munde

9.      Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

a)     Waziri: Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo

b)    Naibu Waziri: Mhe. Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe

c)     Naibu Waziri: Mhe. James Kinyasi Millya

10.   Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

a)     Waziri: Mhe. Boniface George Simbachawene

b)    Naibu Waziri: Mhe. Denis Lazaro Londo

ll. Wizara ya Kilimo

a)    Waziri: Mhe. Daniel Godfrey Chongolo

b)    Naibu Waziri: Mhe. David Ernest Silinde

12.  Wizara ya Maji

a)                                                      Waziri: Mhe. Jumaa Hamidu Aweso

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Kundo Andrea Mathew

13.  Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

a)                                                      Waziri: Mhe. Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho

14.  Wizara ya Ujenzi

a)                                                      Waziri: Mhe. Abdallah Hamis Ulega

b)                                                      Mhandisi Godfrey Msongwe Kasekenya

2

15.  Wizara ya Uchukuzi

a)                                                      Waziri: Mhe. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. David Mwakiposa Kihenzile

16.  Wizara ya Viwanda na Biashara

a)                                                      Waziri: Mhe. Judith Salvio Kapinga

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Patrobas Paschal Katambi

17.  Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

a)                                                      Waziri: Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Switbert Zacharia Mkama

18.  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum

a)                                                      Waziri: Mhe. Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Maryprisca Winfried Mahundi

19.  Wizara ya Afya

a)                                                      Waziri: Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Dkt. Florence George Samizi

20.  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

a)                                                      Waziri: Mhe. Prof. Adolf Faustine Mkenda

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Wanu Hafidh Ameir

21.  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

a)                                                      Waziri: Mhe. Dkt. Leonard Douglas Akwilapo

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Kaspar Kaspar Mmuya

22.  Wizara ya Maliasili na Utalii

a)                                                      Waziri: Mhe. Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Hamad Hassan Chande

23.  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

a)                                                      Waziri: Prof. Palamagamba John Kabudi

b)                                                      Naibu Waziri: Mhe. Hamisi Mwinjuma

c)                                                      Paul Christian Makonda

3


24.  Wizara ya Mifugo na Uvuvi

a)     Waziri: Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa

b)    Naibu Waziri: Mhe. Ng'wasi Damas Kamani

25.  Wizara ya Madini

a)    Waziri: Mhe. Anthony Peter Mavunde

b)    Naibu Waziri: Mhe. Dkt. Steven Lemomo Kiruswa

26.  Wizara ya Nishati

a)     Waziri: Mhe. Deogratius John Ndejembi

b)    Naibu Waziri: Mhe. Salome Wycliffe Makamba

27.  Wizara ya Katiba na Sheria

a)    Waziri: Mhe. Juma Zuberi Homera

b)    Naibu Waziri: Mhe. Zainabu Athman Katimba


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi