Rais Dk.Samia aapisha mawaziri, awaonya
Mwandishi Wetu,
daimatznews@gmail.com
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri aliowateua jana, hafla iliyofanyika leo Novemba 18, 2025, Ikulu Chamwino jijini Dodoma akiwataka kwenda kuwajibika na kuonya haoni tabu kubadili mawaziri.
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Profesa Rikizi Shemdoe akiapa mbele ya Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma leo Novemba 18, 2025. |
Akizungumza
katika hafla hiyo, Rais Samia amesema mawaziri na manaibu wao hao wamekabidhiwa
majukumu ya kuwatumikia wananchi, akiwataka kutanguliza utu na uwajibikaji miongoni
mwao na mbele ya wananchi.
”Kazi ya
kuanzia sasa ni kuendelea kuwajibika kwa Taifa, viongozi wazito punguzeni uzito
ili kwenda sambamba na kasi ya utekelezaji kwa kuwa muda ni mchache,” amesema.
Kwa mujibu wa
Rais Samia, Serikali ya Awamu ya Sita anayoiongoza imepanga kuanza kutekeleza
miradi kwa kutumia fedha za ndani na mashirika ya maendeleo yawakute wameshaanza utekelezaji, hatua inayolenga
kuepusha ucheleweshaji wa miradi kutokana na masharti ya washirika.
Amesema utekelezaji
wa miradi ni jukumu la viongozi wote na si jukumu la Rais pekee na kwamba miradi
yote inapaswa kutoa matokeo chanya kwa kuwafikia wananchi na si kubaki ofisini
kwake.
Pichani
chini;
Rais Dk.
Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mawaziri wa Wizara mbalimbali aliowateua jana.
Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo Jumanne 18 Novemba,
2025.





Maoni
Chapisha Maoni