Miradi ya NHC Kijichi, Kawe 711, Kariakoo nguzo 3 za kipekee Dar
-Kitovu cha mapato NHC, maisha bora kwa wananchi
-Mwanzo mpya wa makazi ya kisasa Dar
-Usanifu unaoendana na Dira ya Taifa ya 2050
-Ubia sekta
binafsi, ubunifu wa NHC vyafungua milango fursa mpya kiuchumi, kijamii
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuthibitisha nafasi yake kama mhimili wa
mageuzi ya sekta ya makazi nchini. Kupitia miradi mikubwa ya kisasa maeneo
mbalimbali nchini, NHC inaonyesha dhamira yake ya kuunga mkono ajenda ya
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha
Watanzania wanapata makazi bora, salama na endelevu.
![]() |
| Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Hamad Abdallah |

Mradi
huu wa Samia Housing Scheme Kijichi unaendelea kwa kasi na ubora wa hali ya
juu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Serikali ya kuongeza wigo wa
makazi bora nchini. Ujenzi wake unafanyika katika eneo la Kijichi na umeleta
mwanga mpya wa maendeleo na hamasa ya kiuchumi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Sifa tano maalum
Mradi wa Samia Scheme Kijichi, umebeba sifa lukuki za kipekee kwa nyumba za makazi, lakini leo tunaweka hadharani sifa tano pekee ambazo ni pamoja na; mgawanyo wa nyumba za kisasa kwa familia tofauti yaani nyumba za vyumba 1, 2 na 3,vilivyopangwa katika majengo 12 ili kukidhi mahitaji ya familia mbalimbali.
| Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi kwenye Mradi wa Samia Housing Scheme Kijichi |
Sifa ya tatu ya Samia Housing Kijichi ni maegesho ya magari takribani 300, yakiwemo maegesho maalum ya ziada kwa ajili ya wageni na dharura.Hapo kila nyumba ina eneo la kuegesha gari yale ya ziada ni 40.
Mradi huo wa Samia Housing Scheme Kijichi una sifa ya nne ambayo ni kuwepo kwa jengo la huduma za kijamii likijumuisha maduka, huduma za kifedha, sehemu za burudani, na maeneo ya michezo kwa familia.
Wakati sifa ya
tano ni ujenzi unaotumia teknolojia rafiki kwa mazingira, ili kupunguza
gharama za ujenzi, kuongeza uimara na kuimarisha usalama wa wakazi.
Sifa hizo zote zinafanya eneo hilo la Kijichi kubadilika na kuwa la kisasa, hivyo hadhi yake na thamani kupanda hata ya maeneo nje ya mradi huo kuongezeka. Sifa hizo zinafanya mradi huo maeneo salama ya kuvutia yanayofaa kwa watanzania wenye kipato cha kawaida na cha kati kununua nyumba hizo bora na kuishi.
| Mradi wa Samia Housing Scheme Kijichi utakavyooneka baada ya kukamilika |
KAWE 711
Mradi wa Kawe 711 ni moja ya alama mpya zinazoinua hadhi ya Dar es Salaam kama jiji la kisasa. Ujenzi wake wa ghorofa 17 kwa kila jengo umefikia zaidi ya asilimia 60, ukichagizwa na mahitaji makubwa ya Watanzania wanaotaka kuishi katika maeneo salama, yenye mandhari mazuri na huduma za kisasa.
Sifa tano maalum
Sifa ya kwanza ya kipekee ya mradi huu ni kuwa na majengo marefu ya kisasa ya ghorofa 17 yaliyo na teknolojia ya kisasa ya ujenzi na usanifu wa kimataifa.
Ya pili ni kuwa na nyumba za hadhi ya juu za vyumba 2, 3 na 4 kupitia mpangilio wa nafasi uliojaa ubunifu zisizochoka zuzitazama.
Sifa ya tatu ya Mradi wa Kawe 711 ni kuwa na maeneo ya burudani na afya ikiwemo mabwawa ya kuogelea, maeneo ya mazoezi, sehemu za watoto na bustani.
Kawe 711 pia
umebeba sifa ya kipekee ya kuwa na maeneo ya huduma za kibiashara ndani ya
mradi ambazo ni maduka, huduma za kibenki na maeneo ya ofisi ndogo.
Maegesho ya
kutosha kwa wakazi wote ndiyo sifa ya tano inayojumuisha maegesho ya
wageni na nafasi za ziada kwa magari ya familia.
Kawe 711 ni
mradi unaolenga familia zinazotafuta ubora wa maisha, ukichangia pia ongezeko
la thamani ya ardhi inayochochewa na shughuli za kiuchumi katika eneo la Kawe
na viunga vyake hivyo kuwa eneo linalofaa kununua nyumba kwa ajili ya makazi
kwa watu wenye kipato cha kati.
Mradi wa Ubia Kariakoo
Mradi huu unaotekelezwa kwa ubia kati ya NHC na wawekezaji binafsi ni mfano bora wa namna ushirikiano unavyoweza kuongeza kasi ya maendeleo ya miji.
Kupitia
mikataba 21, maeneo ya zamani yanageuzwa kuwa miradi ya kisasa yenye matumizi
mchanganyiko yakivutia wafanyabiashara wengi zaidi na kuongezeka kwa shughuli
mbalimbali za kiuchumi.
Sifa tano maalum Sifa kuu za kipekee katika mradi huu ni kuwepo kwa mchanganyiko wa matumizi ya majengo, yaani makazi, biashara, ofisi na huduma mbalimbali katika eneo moja.
Pili, ujenzi
wake ni ule unaoongeza thamani ya Kariakoo kama kitovu cha biashara,
ili kuimarisha uchumi wa eneo hilo.
Sifa ya tatu ni
ubunifu wa usanifu, ambapo una majengo yenye nafasi pana ya kutosha,
usalama, taa za kisasa na mfumo wa usimamizi wa taka.
Mradi wa Ubia
Kariakoo ubejikita katika sifa ya kuwa na uwekezaji unaozalisha mapato mapema,
taarifa za NHC kitengo cha miradi ya ubia zinaonesha kwamba miradi
inayoetekelzwa eneo hilo imeanza kuingiza mapato kabla ya ratiba. Hii ni ishara
ya ubora wa usimamizi wa NHC.
Si hizo tu,
bali sifa ya tano ya Mradi wa Ubia Kariakoo ni kutoa fursa kwa wawekezaji zaidi
ya 100,walioonyesha nia kufanya biashara kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba
la Taifa(NHC). Hii inaonesha kwamba imani ya sekta binafsi kwa NHC imeongezeka.
Mradi wa Ubia
Kariakoo ni chachu ya mageuzi ya maeneo ya biashara Dar es Salaam na utakuwa
nguzo muhimu katika kuongeza mapato ya NHC lakini pia Serikali kupitia kodi,
gawio na shughuli za uchumi.
NHC na kizazi kipya
Kwa ujumla miradi ya Kijichi, Kawe 711 na ya Ubia Kariakoo ni uthibitisho wa jinsi Tanzania inavyopiga hatua kubwa kwenye sekta ya makazi kupitia ubunifu, ushirikiano na uwekezaji wenye tija.
Kupitia miradi hiyo na mengine inayotekelezwa nchi nzima, NHC imejipambanua kama mshirika imara wawekezaji binafsi, pia wa Serikali ikiweka msingi wa miji ya kisasa, yenye usalama, ustaarabu na fursa nyingi za kiuchumi.
![]() |
| Ramani inayonesha maeneo yenye miradi ya NHC mikoa mbalimbali nchini |
Kwa kuongozwa
na NHC ni wazi kwamba, makazi bora si ndoto tena, yanajengwa kila siku na
kizazi kijacho kitaishi katika Tanzania iliyo bora zaidi, salama zaidi na yenye
maendeleo ya kudumu.




Maoni
Chapisha Maoni