Tanzania, Canada kushirikiana kuendeleza sekta ya madini

▪️Balozi wa Canada apongeza mageuzi madini ▪️Wachimbaji wadogo kujengewa uwezo Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com Waziri wa Madini Anthony Mavunde na Balozi wa Canada nchini Tanzania Emily Burns lwamekutana jijini Dodoma na kufanya kikao kuhusu maendeleo ya sekta ya madini nchini. Waziri wa Madini Anthony Mavunde (Kushoto) na Balozi wa Canada nchini Tanzania Emily Burns walipokutana jijini Dodoma na kufanya kikao kuhusu maendeleo ya sekta ya madini nchini. Balozi Emily Burns pia ametumia kikao hicho kujitambulisha, amesema Canada ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika kuwaendeleza wachimbaji wadogo nchini kwa kuwajengeza uwezo katika uchimbaji wa matumizi sahihi ya teknolojia, utakaozingatia utunzaji wa mazingira na kuwajengea ujuzi, ili kuongeza tija kwenye uzalishaji madini. Balozi Burns ameonesha utayari wa Serikali ya Canada kutoa mafunzo maalum (Tailor-made training) kwa wakinamama na vijana kupitia vyuo vya Ufundi-VETA katika maeneo ambayo uzalishaji madini unafanyika...