Serikali yatunga kanuni kuzuia wageni kuingia kiholela leseni ndogo za uchimbaji

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akisoma hotuba
 ya bajeti ya wizara yake bungeni mjini Dodoma.
 
Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Serikali kupitia Wizara ya Madini imetunga kanuni za msaada wa kiufundi katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini ambazo zitaratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo za uchimbaji wa Madini(PML) ambazo kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Sheria ya Madini sura ya 123,kimezitamka Leseni hizi kama maalum kwa ajili ya Watanzania.

Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Madini kinatoa ruhusa kwa mmiliki wa Leseni ndogo ya uchimbaji madini kuingia ubia na mgeni kwa makubaliano ya msaada wa kiufundi (𝙏𝙚𝙘𝙝𝙣𝙞𝙘𝙖𝙡 𝙎𝙪𝙥𝙥𝙤𝙧𝙩).

Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka 2024/25 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Serikali inatarajia kutunga kanuni za kuratibu ushiriki wa wageni katika Leseni ndogo kwa kuwa kumejitokea wimbi kubwa la wageni kuingia katika maeneo ya wachimbaji wadogo kwa mgongo wa “Msaada wa Kiufundi”ambao haukuwa na utaratibu mzuri, hivyo kusababisha wachimbaji wadogo kukosa manufaa yaliyokusudiwa.

Manufaa hayo ni pamoja na kujiimarisha kupitia Leseni ndogo za uchimbaji na wakati mwingine katika vikundi vya wachimbaji viongozi wachache kuingia makubaliano ya msaada wa kiufundi bila kushirikisha wahusika wote na hivyo kuzua migogoro isiyo na sababu.

Tayari Aprili 25.04.2025 Gazeti la Serikali limetoa Tangazo Namba. 260 kuitambulisha kanuni hizo mpya kuanza utekelezaji wake, ikiwa ni ahadi ya Waziri Mavunde akitekeleza maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Kanuni hiyo imetaja mambo mbalimbali muhimu,baadhi yakiwa ni;

1. Usajili wa Mikataba ya Kiufundi kwenye Tume ya Madini baina ya Mchimbaji Mdogo na Mtoa Msaada wa kiufundi.

2. ⁠Kufafanua maana ya maneno “Msaada wa Kiufundi” ili kutimiza lengo mahsusi la kuongeza tija ya uzalishaji na kukuza ujuzi.

3. ⁠Mgawanyo wa Mapato kati ya Mwenye Leseni Ndogo na Mtoa msaada wa Kiufundi kwa madini yatakayozalishwa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Sanamu ya Bikira Maria yaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Saadani

Kapteni Traole afuata huduma za afya nchini

Wawekezaji wa Oman watua nchini, wateta na NHC kuchochea mapinduzi sekta ya makazi