Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com
SAME. Askofu wa Jimbo Katoliki Same, Mhashamu Rogath Kimaryo CSSP, ameshangazwa na tabia ya watu kushabikia neno ubaya ubwela, akilielezea kuwa linayoonesha watu wanafurahia ubaya zaidi kuliko wema.
![]() |
Mhashamu Rogath Kimaryo (CSSP) |
“Hiyo yote ilitokana na watu kushabikia ubaya. Yeyote anayeshabikia ubaya, lazima utakuja kumrudia,” amesema Askofu.\Amefafanua kuwa mahali pa kazi, tabia ya ubaya ubwela ndio husababisha watu kushindwa kufuata maadili ya kazi zao na kusababisha kupeana tuhuma mbaya zikiwamo za ugaidi.
"Ninayasema haya nikiwa na ushahidi kwamba yametokea. Mtu anapewa tuhuma za ugadi, baada ya muda anatolewa kwamba kesi imefutwa. Ni kwamba, hawakuwa na hoja, hiyo ni ukosefu wa maadili na kuua taaluma kwa sababu watu wanashabikia na kuusifu ubaya. Hakuna kitu kibaya kama ubaya," amesema Askofu Kimario. Ameongeza kuwa katika taaluma zote, hapakosi somo la maadili, lakini baadae watu wanakosea taaluma zao na kushabikia ubaya.
"Mnaandaa kesi nje ya hakimu, baadae unasikia ni kweli na vyombo vya habari vinatangaza, fulani ni gaidi, kwenye ubaya gaidi ni neno baya sana sawa na uhaini," amesema
Askofu Kimario amebainisha kuwa kesi hiyo ya ugaidi ilipamba moto, hata yeye asiyekuwa msomi wa mambo ya kipolisi alijua masuala ya PGO (Police General Order), ambayo ingefuatwa mwanasheria angehoji, lakini kwa sababu hayakufuatwa maadili ya kazi, Serikali ikatangaza kutoendelea na hiyo kesi.
"Sasa hutaki kuendelea na kesi wakati mtu umeshamfunga miezi zaidi ya nane, hayo ni maadili kweli? Ni tuhuma tu, ina maana huna hoja, limetumika neno kubwa sana ugaidi."amesema Askofu Kimario.Amesema Watanzania wengi hawapendi kuambiwa ukweli, hasa wanasiasa na kwamba kuna maadili ya siasa hayafuatwi. Cha kuzingatia ni kuacha kutumia maneno mabaya, maana yanaumba. Mfano unapomuita mwanao mbwa, atakuwa tu kama mbwa.
0 Maoni