Hot Posts

6/recent/ticker-posts

Dk.Nchimbi amuomba kura Lissu, Chadema

-Ni iwapo watagomea uchaguzi

-Asema ni haki yao kutogombea 

Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Emmanuel Nchimbi, (Pichani) amekishauri Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutopoteza haki zao zote za kushiriki katika uchaguzi mkuu, Oktoba mwaka huu ambayo ni ya kikatiba kwa kupiga kura au kuchaguliwa, badala yake chama hicho kutumia walau haki moja ya kupiga kura kwa kuipigia kura CCM.

Dk. Nchimbi ametoa kauli hjiyo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), unaofanyika Aprili 4 na 5 Songea Mkoani Ruvuma, ambapo alikuwa mgeni rasmi.

“Angalau katika hizo haki mbili ndugu yangu Tundu Lissu hakikisha unaipata mojawapo. Ukishindwa kuchaguliwa basi chagua. Unakuwa umetutendekea haki na ninaamini rafiki yangu Tundu Lissu na wenzake haki ya kuchagua wataitumia vizuri. Naminaomba kura zenu,” amesema Dk. Nchimbi na kufafanua:

“Kugombea na kutogombea vyote ni sawa ni haki yao kikatiba; ...Hata hivyo kama watagomea wasisahau kura zao au sio… ndio jadi yetu kwani ukikosa haki ya kuchaguliwa usipoteze haki ya kuchagua.

Amesema kwa mujibu wa Katiba, hata kama chama kikiwa kimoja shiriki, kuhakikisha wananchi watapiga kura ya ndio au hapana. 

Nchimbi ambaye pia ni mgombea mwenza Mteule wa nafasi ya umakamu wa Rais kwa tiketi ya CCM ameonya kuwa kuwasemasema CHADEMA sio sawa.

“Kwa hiyo namwambia rafiki yangu Tundu Lissu anahaki ya kuzuia chama chake kutogombea na tutawaunga mkono vyovyote watakavyoamua.

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi (Kulia) akiteta na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, wakati Dk, Nchimbi alipokuwa mgeni rasmi kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa jukwaahilo,mjini Songea, Mkoa wa Ruvuma Aprili 4, 2025/ 

Alikuwa akizungumzia kampeni inayoendeshwa na Chadema maarufu  “No Reform no Election ‘ huku akieleza kuwa hakuna sababu ya kukilazimisha chama hicho kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwani vyovyote watakavyoamua iwe kushiriki au kutoshiriki ni sawa.

Kwa mujibu wa k, Nchimbi ni kosa kukilazimisha chama cha siasa kushiriki uchaguzi huku akibainisha hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kuzuia Uchaguzi Mkuu.

Dk.Nchimbi amesema Tanzania ina utaratibu wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano na hakuna yeyote anayeweza kuzuia uchaguzi usifanyike.

“Hata Rais  hawezi kulitamkia Taifa kuzuia uchaguzi mkuu;  Hilo ni takwa la kikatiba. Nataka niwahakikishie  Watanzania wote kuwa uchaguzi wa madiwani, wabunge na Rais mwaka 2025 utafanyika.”

Dk.Nchimbi amesema pamoja na haki ya kuchagua na kuchaguliwa ni kosa kukilazimisha chama kingine cha siasa kuingia kwenye uchaguzi.


Chapisha Maoni

0 Maoni