Ni Hassan Doyo na Mfaume Khamis
Na Hussein Ndubikile, daimatznews@gmail.com
Chama cha National League for Democracy (NLD) kimetangaza majina ya wagombea urais watakaochuana na wangombea wa chama tawala CCM, katika Uchaguzi Mkuu ujao Oktoba mwaka huu 2025 kikieleza wamefikia hatua hiyo baada ya mchakato wa ndani wa chama hicho kukamilika kwa mafanikio.
Katika mchakato huo NLD kimempitisha Doyo Hassan Doyo kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho huku Mfaume Khamis akiteuliwa kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar.
Tayari CCM kimewapitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwania kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk.Hussein Mwinyi kuwania kiti cha urais visiwani Zanzibar,hivyo sasa watachuana na Doyo na Mfaume Khamis katika kinyang'anyiro hicho,.
"Uamuzi huo umetokana na vikao halali vya chama, kufuata taratibu zote za kikatiba na mapendekezo ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kutoka sehemu mbalimbali kote nchini," imesema NLD.
Chama hicho kimebainisha kuwa kina imani wateule hao kwani ni mfano wa uongozi bora, wenye maono makubwa ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa Watanzania wote na kwamba kimejizatiti kuendeleza misingi ya demokrasia, uzalendo, haki, na maendeleo jumuishi kwa kila Mtanzania.
NLD kimewaomba wanachama na wapenzi wake, na wananchi wote kuwa pamoja katika safari hii ya matumaini na mabadiliko.
0 Maoni