MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI MISA KUMKUMBUKA NYERERE

 Mwandishi Wetu, daimatznews@gmail.com

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi ameshiriki Ibada ya Misa Takatifu ya kumuombea Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi(Kushoto), akisalimiana na Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere. 

Misa hiyo takatifu imefanyika leo Oktoba14,2026 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Epifania, Jimbo Katoliki Sumbawanga kuadhimisha miaka 27  tangu kufariki kwa muasisi huyo wa Tanzania.

Mwalimu Nyerere alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas, jijini London, Uingereza alipolazwa kwa matibabu ya saratani ya damu.

Ibada hiyo, imeongozwa na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga Damian Kyaruzi na kuhudhuriwa pia na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere, pamoja na viongozi, waumini na wananchi mbalimbali.








Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi