WAZIRI MKUU MGENI RASMI MKUTANO MKUU WAAHMADIYA

Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgezi rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka (Jalsa Salana) wa 55 wa Jumuiya ya Wailamu Waahmadiyya nchini utakaofanyika eneo Maarufu la Ahamdiyya liliopo Kitonga, Kata ya Msongola Wilayani Ilala Dar es Salaam, Septemba 25 hadi 27 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari leo Septemba 22,2026 jijini humo, Amir na Mbashiri Mkuu Jumuiya hiyo Sheihk Khawaja Muzaffar Ahamad amesema utaratibu wa kufanyika mkutano ulianzishwa na  Mwanzilishi mtukufu wa jumuiya hiyo Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad.
Amesema mwanzilishi huyo alitumwa na Mwenyezi Mungu kuja kutimiliza bishara za ujjai wa Imam Mahdi pamoja na ujaji wa Masihi katika zama hizi zilivybainishwa na Mtukufu Mtume Muhammad s.a.w na waanzilishi wa dini zingine duniani.

"Mkutano huu unafanyika ili kuongeza hofu ya Mwenyezi Mungu mioyoni mwa washiriki kupata Taqwa, kumjali Mungu, kuepukana  na mabaya, kupata moyo wa huruma na kuongeza upendo baina yao," amesema Sheikh Khawaja.

Amebainisha kuwa kenye mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, viongozi wa dini na viongozi wa kijamii kwa ujumla lengo likiwa kutoa nasaha zao.

Amesisitiza kuwa kauli ya Jalsa Salana ya maku ni Taqwa (uchamungu) ndio mzizi wa kila wema ikilenga kuwakaumbusha waumini juu ya ualazima wa kuipata taqwa kwa kutekeleza maamrisho yote ya Mwnyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake yote, sio kwa lengo lolote bali kupata radhi na mapenzi ya Mungu tu.
Amefafanua kuwa mkutano huu utahudhuriwa na washiriki 5500 kutoka maeneo mbalimbali kutoka nchini na nje ya nchi na kwamba hotuba na nasaha za wataalamu wa jumuiya hiyo zitatolewa ikiwemo maisha Mtume Muhammad s.a.w kuwa ni Chemchem ya Taqwq nq uchamungu, jinsi ya maisha ya mafundisho ya masihi na malezi bora ya familia pamoja na mafanikio katika maisha ya mtu.

Pia amesema washiriki wenye afya zao na rika linalorhusiwa watapata nafasi ya kuchangia damu kwenye Benki ya Taifa ya Damu Salama huku akikazia hotuba zote za Jalsa Salana ya mwaka huu zitasikika mubashara kupitia redio ya Ahmadiyya Mtwara na tovuti ya redio hiyo inayojulikana https: //www.radioahmadiyya.or.tz.

Sheihk Khawaja lengo la jumuiya hiyo ni kutangaza amani kwa ujumbe sahihi wa waislamu duniani kote na kuwa mstari wa mbele kupinga amani zisizo sahihi za mawazo zinazobainishwa na uislamu ikiwaemo jihadi ya upanga, ugaidi, kutokutii serikali zisizo za kiisalmu pamoja na kuwa misimamo mikali isiyovumilia wengine.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi