KADOGOSA WAZIRI WA UJENZI

 Mwandishi Wetu,daimatznews@gmail.com

Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Masanja Kadogosa(Mb),kuwa Waziri wa Ujenzi.

Waziri wa Ujenzi Mteule, Masanja Kadogosa.

Taarifa iliyotewa leo Septemba 27,2026 na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bakari Machumu, imemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka kwamba,Rais Samia pia amemteua Abdalah Ulega kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. 

Kabla uteuzi huo Ulega alikuwa Waziri wa Ujenzi, huku pia Rais akimteua Juma Homela kuwa Waziri wa Nishati akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Deogratius Ndijembi ambaye sasa ni Makamu wa Rais.Homela alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Taarifa zaidi soma hapa chini...




Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi