HANSPAUL GROUP YASHINDA TUZO NNE PMAYA 2026

-Yampongeza Rais Samia kuendelea kutetea Sekta Binafsi

Hussein Ndubikile, daimatznews@gmail.com
Kampuni ya Hanspaul Group imeng'ara katika Hafla ya 19 ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Mwaka ( PMAYA) kwa kufanikiwa kushinda jumla ya Tuzo nne zinazoandaliwa na Shirikisho la Viwanda Tanzania(CTI).

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kupokea tuzo hizo, Mkururugenzi Mtendaji wa Kampuni HanPaul, Satbir Singh Haspaul amemshukuru na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutetea sekta binafsi na kwa CTI.

"Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Rais Samia kwa kutetea sekta binafsi Tanzania na CTI, Serikali ya Tanzania na Wizara zetu husika kwa msaada wanaoendelea kuutoa, " amesema Hanspaul.

Amebainisha kuwa ushindi wa tuzo unakwenda kwa wateja wao na kwamba umetokana na ushirikiano wanaoupata kutoka washirika na wadau wote ambao wana imani ya kujitolea hali inayowachangia kupata mafanikio.

Amesisitiza kuwa ushindi wa tuzo hizo unaendeleza rekodi nzuri ya kampuni hiyo katika utengenezaji wa miundo ya chuma, maboksi, pamoja na uundaji wa karakana za magari ya utalii na teknolojia ya kubadili magari ya mafuta kwenda mifumo ya umeme nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hanspaul Group amepokea tuzo nne zinazoyatangaza na kuyatambua makampuni tanzu ikiwemo Dharam Singh Hanspaul & Sons Limited, Hanspaul Industries Ltd, Hanspaul Automechs Ltd pamoja na E- Motions Ltd.

Post a Comment

Mpya zaidi Nzee zaidi